Monday, May 07, 2018

TANZANIA CHIMBUKO LA BINADAMU WA KWANZA, NI BUSTANI YA EDEN



Hatimaye utata uliokuwa ukiendelea duniani kwa watafiti wa mambo ya kale kuhusiana na mahali mwanadamu wa kwanza alipotokea umemalizika baada ya jopo la wataalam liloundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia ushahidi wa vinasaba kubaini kuwa binadamu huyo alitokea barani Afrika huku ikidaiwa kuwa ni Tanzania eneo la Olduvai Gorge.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya ufugaji nyuki aloiutisha kujadili maendeleo ya sekta hiyo Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Amesema utafiti huo umeshirikisha wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani na kuwa kumalizika kwake kutaiwezesha sekta ya utalii nchini kukua kwa kasi sambamba na kuongeza pato la taifa.


No comments:

Post a Comment