Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Vertiv imefanya maboresho ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vinavyotumika katika ujenzi, viwandani na maofisini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati yao wamiliki wa viwanda na kampuni mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza jana Dar es Salaam, katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Rais wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk alisema kuwa wamefanya maboresho ya bidhaa zao ili kusaidia wateja wao kujua endapo vifaa vyao vimepata hitilafu au la.
Amesema bidhaa wanazozizalisha ni pamoja na vifaa vya kudhibiti nguvu ya umeme, Ac zinazotumika kwenye viwanda, UPS na ambazo zimewekewa uwezo wa kutoa taarifa kwa mtumiaji kama kifaa anachotumia kimeshindwa kufanya kazi kwa sababu gani.
‘’Tumefanya maboresho kwa bidhaa zetu ambapo wenye vituo vya data kama vile kampuni za simu, ofisi za serikali na kampuni binafsi watapata taarifa kuonesha kuwa kama UPS au AC za viwandani hazifanyi kazi kwa sababu ya umeme mdogo au kuna tatizo lingine ambalo linapaswa kufanyiwa marekebisho,’’ amefafanua Wyk.
Amesisitiza kuwa wanaendelea kuboresha bidhaa hizo ambazo zinatumika katika nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki (EAC) na Ulaya kwa kuwa wanaamini ukuaji wa teknolojia unasaidia katika kuleta maendeleo chanya kwa kila nchi.
Naye mshirika wa kibiashara na Mtaalamu wa masula ya mawasiliano, Mihayo Wilmore amesema kuwa uboreshaji wa vifaa hivyo utasaidia maeneo mengi ikiwemo hospitalini na maofisini ambako matumizi makubwa ya teknolojia hufanyika.
Amesema kuwa watu wanaotumia mitambo mbalimbali katika shughuli zao, ni muhimu kujua ni muda gani vifaa vyao vimeweza kuzimika kwa sababu ya kuisha kwa umeme, hutupata ujumbe mfupi wa maandishi kuelezea tatizo lililotokea.
‘’Ni muhimu kwa hospitali kujua UPS wanayotumia inaweza kuzimika kwa muda gani na sababu gani zinazosababisha jenereta kuzimika hii itasaidia kurahisisha utoaji wa huduma haraka. Pia wameonesha uwezo wa kutengeneza vituo vya data katika simu au kompyuta ili kutoa taarifa kwa haraka kwa wateja wao,’’ ameeleza Wilmore.
Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano kutoka Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, Johan Terblanche akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake juu ya umuhimu wa UPS kutoka Vertiv katika Data Centre.
Mkurugenzi wa huduma wa Vertiv Mashariki ya Kati , Pascal Bodin akieleza namna kampuni hiyo ilivyoweza kunufaisha Viwanda vya ukanda huo.
Mshirika wa kibiashara wa Elcom Solution ambao wamewakaribisha Vertiv nchini, Mihayo Wilmore akieleza Waandishi wa Habari umuhimu wa mitambo ya Vertiv katika sekta ya Afya nchini.
Wakurugenzi wa EL- COM Solutions , Deen Nathwani, Jimy Apson na Amin Valji wakizungumza jambo wakati wa Warsha wa kutambuslisha bidhaa za Vertiv nchini.
Wafanyakazi wa Vertiv wakiwa katika picha ya pamoja na Washirika wao El-com Solution na washirika wengine kutoka nchini Kenya mara baada ya kumaliza warsha ya kutambulisha bidhaa zao Tanzania
No comments:
Post a Comment