Sunday, February 04, 2018
MHE BITEKO AWATAKA VIONGOZI CCM KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI
PICHANI: Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita akisisitiza jambo wakati akihutubia mamia ya wanachama kwenye maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Na Mathias Canal, Geita
Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Februari 4 kila mwaka huadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa Chama hicho kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) Februari 5 mwaka 1977.
Kutokana na umuhimu wa maadhimisho hayo Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamehimizwa kuwa na ujasiri wa kuisimamia vyema serikali ili kutatua matatizo yanayowakabili wananchi katika jamii ili kuakisi mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya ushindi ya mwaka 2015-2020.
Kauli hiyo imetolewa leo 4 Februari 2018 na Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita wakati akihutubia mamia ya wanachama waliohudhuria maadhimisho hayo yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente.
Mhe Biteko alisema kuwa kumekuwa na undumilakuwi kwa baadhi ya viongozi wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotokana na kujisahau na kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo linachochea hisia kali kwa wananchi dhidi ya serikali yao kutokana na watendaji wachache waliopewa dhamana kutotekeleza vyema majukumu yao.Akizungumza kwa hisia chanya Naibu waziri huyo alisema kuwa maadhimisho ya CCM ni muhimu katika Taifa kwani Tendo hilo la kihistoria ni maalumu kwa ajili ya kuendeleza utamaduni uliokuwa umeanza huko nyuma wa kuunganisha nguvu kwa lengo la kujiimarisha katika mapambano. Kwa mfano, ASP kwa upande wa Zanzibar ilitokana na kuungana kwa African Association (AA) na Shirazi Association (SA), tendo ambalo liliunganisha nguvu za wanyonge katika mapambano ya kuundoa usultani na utawala wa kikoloni wa Kiingereza.
Alisema kuwa kwa upande wa Tanzania Bara, TANU ilitokana na kujibadilisha kwa Tanganyika African Association (TAA) kutoka jumuiya ya kutetea maslahi ya kijamii na kuwa chama cha siasa ambapo muunganiko wake uliibua mapambano ya ukombozi katika Afrika na kote duniani kujenga Tanganyika na Zanzibar huru kiuchumi na kijamii na kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.
Aidha, alisiitiza kuwa wananchama wanapaswa kuvunja makundi mbalimbali yanayoibua hisia hasi za utengano ambazo zinatokana na chuki dhidi ya wananchama wengine, chuki dhidi ya viongozi wa chama na serikali, badala yake kukiri kwa kauli moja kuwa Umoja ni Nguvu na Utengano ni udhaifu hivyo kutokuwa na chuki za daima kwani katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu.
Alisema kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi wote wanapaswa kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ndiye kiongozi mkuu wa serikali, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwani amekiwezesha Chama Cha Mapinduzi kuwa Chama chenye nguvu, imara na madhubuti, hivyo kuwa Chama cha siasa pekee chenye uwezo wa hali ya juu wa kuwaunganisha Watanzania.
Mhe Mashaka Doto Biteko Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Naibu Waziri wa Madini, alisema kuwa Rais Magufuli ameiwezesha CCM kuwaongoza wananchi katika mapambano ya kitaifa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kufuatana na mabadiliko mbalimbali yanayojitokeza ndani na nje ya nchi.
Sambamba na hayo pia Mhe Biteko amesifu juhudi hizo za Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kukiongoza vyema Chama hicho na hatimaye kuendelea kuungwa mkono na CCM kuendelea kupewa dhamana na wananchi ya kuunda serikali na kukamata dola tangu 1977 chini ya mfumo wa demokrasia ya chama kimoja hadi sasa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, kufuatia mageuzi yaliyoidhinishwa na marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania Juni 1992.
Maadhimisho ya miaka 41 ya CCM Mkoani Geita yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Geita Alhaji Said Karidushi ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Katibu wa CCM Mkoa wa Geita Ndg Adam Ngalawa, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel, na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na serikali ngazi ya Mkoa, na Wilaya.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018.
Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini Mkoani Geita wakifatilia kwa makini maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe akimualika aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuely Lwehahula kuwasabahi wanachama wa CCM wakati wa maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018.
Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini Mkoani Geita wakifatilia kwa makini maadhimisho ya miaka 41 ya CCM yaliyofanyika Kimkoa katika eneo la Ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliopo Kijijini Mtambala Kata ya Katente, Wilayani Bukombe, Leo 4 Februari 2018.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment