Thursday, November 23, 2017

NAIBU WAZIRI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATEMBELEA TTCL, AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akisaini kitabu cha wageni alipofika Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi mbalimbali zilizoko katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika wizara hiyo, Mhandisi Clarence Ichwekeleza na wengine ni baadhi ya Maofisa wa wizara hiyo.





Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba akimweleza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia), jinsi taasisi hiyo, inavyotekeleza majukumu yake ya kiutendaji na hatua zinazochukuliwa katika kulipatia mafanikio zaidi.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakati wa ziara yake hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba.


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na uongozi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakati wa ziara yake hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akielezea jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), katika ziara hiyo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba (aliyesimama) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa wizara yake, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, wakifuatilia mazungumzo kati yake na wafanyakazi wa TTCL mjini Dodoma kwa njia ya Video Conference.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na wafanyakazi wa TTCL mjini Dodoma kwa njia ya Video Conference, wakati wa ziara yake akiwa TTCL Makao Makuu Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba (aliyesimama) na baadhi ya Maofisa wa wizara yake, wakisikiliza maelezo ya wafanyakazi wa TTCL wa mjini Dodoma,wakati akizungumza nao katika mkutano huo, kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam leo.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia waliokaa), Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika wizara hiyo, Mhandisi Clarence Ichwekeleza (kushoto waliokaa) na baadhi ya Maofisa wa Wizara na wa Kampuni ya TTCL.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto), akipatiwa maelezo kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa huduma ya Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa na Mhandisi Amani Kichere wa TTCL, wakati wa ziara yake hiyo, jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto), akipatiwa maelezo na Mhandisi Amani Kichere wa TTCL, kuhusu kifaa maalum kinacholinda usalama wa wataalamu wakati wanaposhughulikia mitambo ya Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa katika ziara yake hiyo, leo jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akipatiwa maelezo kuhusu huduma ya TTCL Pesa kwenye duka la taasisi hiyo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba wakati wa ziara yake hiyo, Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akiongea na mteja kuhusu huduma za TTCL kwenye duka la taasisi hiyo, wakati wa ziara yake jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akipatiwa maelezo na mmoja wa wafanyakazi wa duka la TTCL, wakati alipotembelea duka hilo, katika ziara yake hiyo, Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment