Monday, October 16, 2017

TANESCO KUTUMIA WATALAMU WAKE KUJENGA VITUO NA NJIA ZA KUSAFIRISHA UMEME


 


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, Lindi

KATIKA kutekeleza dhana ya kujenga uzalendo na kubana matumizi, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia kampuni yake tanzu ya ETDCO, limeanza kutumia wataalamu wake wa ndani kujenga vutuo na njia za kusafirisha umeme.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, (Transmission), Mhandisi Kahitwa Bishaija,(pichani juu), amesema kwa kuanzia, TANESCO ilitumia wahandisi na mafundi wake kujenga kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 132kv cha Mtwara na kingine cha Mahumbika Mkoani Lindi ikiwa ni pamoja na kujenga njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 132Kv yenye urefu wa kilomita 80 kutoka Mtwara hadi Mahumbika.

“Huu ni mwanzo mzuri kwetu tunaendelea kujenga vituo vingine na kituo kinachofuata kwenye mpango ni kile cha Kimbiji, wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.” Alisema Mhandisi Bishaija wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea miundombinu ya TANESCO, kwenye mikoa ya Njombe, Songea, Mtwara na Lindi iliyofikia kilele Oktoba 16, 2017.

Akifafanua zaidi kuhusu azma hiyo ya Shirika, Mhandisi Bishaija alisema, miradi hiyo ya umeme ya Mtwara na Mahumbika, licha ya kukamilika ndani ya kipindi kifupi, lakini pia imekuwa ya ubora wa juu.

“TANESCO ilitumia uwezo (capacity) wa ndani kwa maana ya fedha, wahandisi na mafundi lakini pia hata jamii zinazozunguka vituo ndio walioshirikiana na mafundi wetu katika ujenzi wa vituo na njia hii ya kusafirisha umeme, na hakika mafanikio haya ndiyo yametupa ujasiri wa kuwa na mipango endelevu ya jkuendelea kutumia uwezo wetu sisi wenyewe.” Alisisitiza Mhandisi Bishaija.

Aidha Meneja wa TANESCO Mkoani Lindi Mhandisi Johnson Mwigune, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Mahumbika, umesaidia kuboresha hali ya umeme hii ni kutokana na urefu wa njia ya umeme kutoka Mtwara kuja Lindi, na kuwepo kwa michepuko mingi na transom nyingi, hitilafu ikitokea kwenye njia hiyo ilikuwa inasabisha mkoa mzima kukosa umeme, lakini sasa hivi matatizo ya katikati ya njia kati ya Mtwara na Lindi hayapo tena kutokana na uwepo wa kituo hiki.


Kituo kipya cha kupoza umeme wa 132kV cha Mahumbika mkoani Lindi kilichojengwa na wahandisi na mafundi wa TANESCO mapema mwaka huu.




Jengo la kituo cha kupoza na kusafirisha umeme wa 132kV cha Mtwara kilichozindukliwa na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Machi 5, 2017.



Meneja Mradi wa uboreshaji umeme mikoa wa Mtwara na Lindi, kutoka kampuni tanzu ya TANESCO, EDCO, Mhandisi Japhary Msuya, akielezea utekelezaji wa miradi hiyo.


Transfoma mpya ya 132/32/Kv 30MVAkituo cha Mtwara.


Hapa ndipo umeme unapochukuliwa kutoka kituo cha Mtwara 132/33Kv kwenda kituo cha Mahumbika, 132/33kV mkoanin Lindi.

Hii ndio kazi iliyofanywa na mafundi wazawa wa TANESCO

Hii ndio kazi iliyofanywa na mafundi wazawa wa TANESCO, ujenzi wa njia (line), ya 132kV kutoka Mtwara kwenda mkoani Lindi.


Mhandisi Bishaija, akizungumza na wahariri kwenye kituo cha kufua umeme utoknao na gesi cha, Mtwara.


Meneja Mradi wa uboreshaji umeme mikoa wa Mtwara na Lindi, kutoka kampuni tanzu ya TANESCO, EDCO, Mhandisi Japhary Msuya, akiwaongoza wahariri kutembelea kituo cha Mtwara Oktoba 15, 2017.


Msimamizi wa kituo cha kudhibiti mfumo wa umeme cha Mtwara, akiwa kazini.


Gesi ikiunguzwa ili kuendesha mashine 8 za kufua umeme kituo cha umeme, Mtwara.


Gesi ikiunguzwa ili kuendesha mashine 8 za kufua umeme kituo cha umeme, Mtwara.


Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usafirishaji umeme, Mhandisi Kahitwa Bishaija, (kulia), akizungumza jambo na msimamizi wa mfumo wa udhibiti umeme kituo cha Mahumbika Bw.Juma Yahya Mshangama Oktoba 15, 2017. Wengine pichani ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi, Mhandisi Johnson Mwigune, na Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO Makao makuu, Bi. Leila Muhaji.






Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi, Mhandisi Johnson Mwigune


Juma Yahya Mshangama-Msimamizi wa mfumo wa udhibiti umeme kituo cha Mahumbika.









No comments:

Post a Comment