Friday, August 04, 2017
UTAFITI: PICHA ZA NGONO NI HATARI, HUADHIRI NGUVU ZA KIUME
Na Mwandishi Wetu,
Picha na video za ngono(pornography) katika mitandao ya intaneti zimekuwa zikisambaa kuliko kawaida, lakini ongezeko la athari linazidi kuangamiza na kuharibu mahusiano ya kweli maishani, jambo ambalo linazidi kuwagusa wanasayansi na kusababisha tafiti mbalimbali kuendelea kufanywa ili kudhibitisha athari hizo.
Katika chapisho la mtandao wa gazeti la kila siku la Independent nchini Uingereza, utafiti unaonesha kuwa matumizi ya video na picha za ngono kupita kiasi una athari mbaya kwa wanaume na huatarisha uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa ripoti ya jarida la News Week, mjadala wa 112 wa kongamano la mwaka la wanasayansi lijulikanalo kama ‘112th Annual Scientific Meeting of the American Urological Association’ limetoa matokeo ya utafiti huo ulioonesha kuwa wanaume wanaopenda picha/vodeo za ngono wako hatarini kupoteza uwezo wa kusimamisha uume.
Kiongozi wa utafiti huo, Dkt. Matthew Christman, ambaye ni mtaalamu wa mishipa ya fahamu kutoka Naval Medical Center, San Diego, nchini Marekani, ameeleza, jinsi mwanaume anavyotumia muda mwingi kuangalia picha na video hizo katika mitandao, ndivyo uwezo wake wa kujihusisha na matukio ya kweli na mwenza wake chumbani unzvyozidi kupungua.
Matokeo yake, mahusiano yanazidi kuwa na changamoto na hata kuadhiri mapenzi na tendo la kujamiiana. Utafiti huo ulihusisha wanaume 312 kati ya umri wa miaka 20 na 40, na kuonesha kuwa matumizi ya picha na video za ngono yaliyopitiliza yanahusiana na kupungua kwa nguvu za kiume. Utafiti pia umeonesha kuwa asilimia 20 ya wanaume huangalia video na picha za ngono kati ya mara 3 mpaka 5 kwa wiki.
Utafiti huo pia umeonesha kuwa asilimia 4 ya wanaume wengi hupendelea zaidi kupiga punyeto kuliko video na picha za ngono dhidi ya kufanya mapenzi na wenza wao. Matokeo ya utafiti huo pia yameonesha kuwa wanaume wengi wanaopendelea video na picha za ngono hukumbwa na tatizo la kukosa hamu ya ngono pamoja na kukosa nguvu za kiume.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment