Wednesday, July 19, 2017
JUMIA TRAVEL YAUNGANISHA MFUMO WA HUDUMA KWA WATEJA NA FACEBOOK MESSENGER
PICHANI: Kampuni inayoongoza kwa uwakala wa huduma za kusafiri mtandaoni Afrika, Jumia Travel imezindua mfumo mpya wa huduma kwa wateja kupitia ‘Facebook Messenger’ kwa kushirikiana na Salesforce (Kampuni kinara kwenye Usimamizi wa Huduma kwa Wateja)
Na Jumia Travel
KATIKA kuboresha utoaji wa huduma Jumia Travel imeuunganisha mfumo wake wa kuwasiliana na wateja kupitia Facebook Messenger. Kuunganishwa kwa ‘Messenger’ kwenye mfumo wa utoaji wa huduma wa Jumia Travel ni ishara ya mapinduzi makubwa kwenye kuwapatia wateja uzoefu, kwani unatoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja kwenye Facebook messenger. Njia hiyo pia inaweza kutumika kuomba huduma ya chumba hotelini papo hapo, ambapo wataalamu wa masuala ya kusafiri wa kampuni watakuwa wakitoa ushauri juu ya machaguo bora zaidi ya malazi pamoja na kufanya huduma.
Ikiwa ni kampuni ya kwanza barani Afrika kuunganisha huduma ya Facebook Messenger kwenye mfumo wake wa utoaji huduma, Estelle Verdier, Afisa Mkuu wa Oparesheni na Mwasisi-mwenza wa Jumia Travel amesema kuwa, “hii ni hatua katika kuonyesha namna tulivyojipanga siku zote kuwaletea wateja wetu teknolojia za kisasa na huduma zenye ubora wa hali juu.”
Kwenye ripoti waliyoizindua hivi karibuni juu ya sekta ya utalii Tanzania, Jumia Travel imebainisha kuwa 65% ya utafutwaji wa huduma za hoteli kwenye mtandao wao hufanyika kupitia simu za mkononi huku 35% ndiyo wanaofanya huduma. Ukulinganisha na wateja wanaoutumia kompyuta 40% hutumia kwa kutafuta huduma wakati 60% ndio wanaofanya huduma.
“Kwa upande wa Afrika, kupenya kwa matumizi ya barua pepe (e-mail) kumekuwa ni kwa kusuasua kutokana na njia hiyo kutotoa fursa ya mazungumzo ya mara kwa mara na haisawiri kwa kiasi kikubwa kwenye simu za mkononi. Kwa kuunganisha utoaji wa huduma na Messenger, tumewaletea wateja wetu njia ya papo kwa papo na rahisi ya kuwasiliana nasi kwenye simu za mkononi kupitia Facebook. Tuna imani kwamba Facebook Messenger itakuwa ni njia kuu kwa miaka ijayo, na kipengele hiki kipya kwetu kitaturuhusu kuongeza namna ya kuwasiliana na wateja wetu kupitia Messenger,” alisema Stanislas Dinechin, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Jumia Travel Kimataifa.
“Kwetu sisi hii ni fursa kubwa kwa kuweza kuunganisha mfumo wetu wa huduma kwa wateja na Facebook Messenger kwa sababu watanzania wengi wanaipata kupitia simu zao za mkononi. Tunatumaini wateja wataupokea mfumo huu mpya na kuutumia vizuri katika kufurahia huduma zetu,” alithibitisha Fatema Dharsee, Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania.
Njia hii pia itakuwa ikitumika kushughulikia masuala na maombi mbalimbali ya wateja kama vile huduma ya usafiri kutoka uwanja wa ndege pamoja na kubadili huduma ya malazi iliyokwishafanyika. Afrika ikiwa na watumiaji wengi wa simu za mkononi, Facebook Messenger inatoa fursa kubwa ya kuwafikia watu wengi ukijumuisha na wa kwenye mitandao mingine ya kijamii ukilinganisha na wanaotokana na kumtembelea mtandaoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment