Wednesday, October 19, 2016

TAASISI YA ADLG YAANZA KUWANOA WANAHABARI JIJINI MWANZA KUHUSIANA NA SEKTA YA MADINI NCHINI


Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza, wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari zenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini.

Pia wanahabari hao walipata wasaa wa kuwasilisha tathimini yao kuhusiana na ziara mbalimbali ambao wamezifanya kwenye maeneo yenye wawekezaji wa madini Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoani Shinyanga.

Wa kwanza kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo, Fredirick Katulanda, ambaye pia ni mhariri wa magazeti ya kampuni ya New Habari (2006) Ltd Kanda ya Ziwa. Mafunzo hayo yanaandaliwa na Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, yenye makao yake makuu Jijini Mwanza.

Na BMG

Na George Binagi-GB Pazzo

Waandishi wa Habari mkoani Mwanza, wameanza kupatiwa mafunzo yatakayowasaidia kuandaa habari, makala pamoja na vipindi vyenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Fredrick Katulanda, amesema hatua hiyo itasaidia kuibua chachu ya wananchi kutambua haki zao kuhusiana na masuala ya uwekezaji wa madini na hivyo kuondoa migogoro iliyopo baina yao na wawekezaji.

Baadhi ya waandishi wa habari wanaonufaika na mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kuandaaji wa habari zenye tija kwa jamii ikiwemo kuondokana na madhara yanayotokana na shughuli za migodini kama vile athari za maji taka.
Mafunzo hayo yanaandaliwa na Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ambapo Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, amesema mafunzo yatawasaidia waandishi wa habari kuibua masuala mbalimbali yenye changamoto katika sekta ya madini ili kutafutiwa ufumbuzi.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, Jimmy Luhende, akifuatilia majadiliano hayo.


Baadhi ya Wanahabari/Bloggers Jijini Mwanza


Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza wakiwa kwenye mjadala mzito kuhusu sekta ya madini nchini.






No comments:

Post a Comment