Baadhi ya Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakitafakari kabla ya kuanza kwa mbio hizo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo akizungumza jambo na Mgeni Rasmi ,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura kabla ya kuanza kwa mashindano ya mbio za Baiskeli. Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Baiskeli Tanzania (CHABATA) Godfrey Mhagama akieleza sheria mbalimbali za mchezo huo kabla ya kuanza rasmi mbio hizo. Asa Mwaipopo ,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ulio chini ya Kampuni ya Acacia ,akizungumza kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yanayofanyika kwa mwaka wa tatu katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga.Wengine kutoka kulia ni
Meneja Uendelevu wa Mgodi wa kuchimba Dhahabu wa Buzwagi,George Mkanza,Mgeni rasmi katika mashindano hayo Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura na katikati ni Katibu wa Baraza la Michezo (BMT) .Said Kiganja.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura akiendesha baiskeli kuashiria kufunguliwa rasmi kwa mashindaano ya Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016.
Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa ameshika bendera ,tayari kuanzisha mbio hizo,kulia ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo.
Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakianza mbio hizo.
Baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Kahama na Vitongoji vyake wakiwa barabarani kushuhudia mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Paomja Cycle 2016.
Mmoja wa waendesha Baiskeli akipewa maji na mmoja wa makamisaa wa mchezo huo Aman Vicent wakati mashindano hayo yakiendelea.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Madini ya Acacia, Necta P Foya akishiriki mashindano hayo kwa upande wa wanawake .
Umati mkubwa wa wananchi wakiwa barabarani wakingojea kumshuhudia mshindi wa mbio za baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Chalange 2016.
Muonekano wa picha ya juu eneo la Phantom eneo ambako mashindano hayo yalianzia na kumalizikia.
Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakihitimisha mbio hizo.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog aliyeko Kahama,Shinyanga.
No comments:
Post a Comment