Tuesday, June 14, 2016

WANA CCM MAHINA WACHACHAMAA, MEYA WA JIJI LA MWANZA KUPULIZIWA HEWA CHAFU OFISINI

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MADAI ya Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire kupuliziwa ofisini kwake juzi hewa chafu inayohisiwa kuwa sumu yamesababisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) wa Kata ya Mahina anakotoka meya huyo kutinga kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana wakishinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa kadhia hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti juu ya tukio hilo wana CCM hao walisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha kupuliziwa sumu kwa Diwani wa Kata ya Mahina na Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire.

Pia wametoa angalizo kwa uongozi wa CCM na serikali ya wilaya kuwa Diwani na Meya huyo wa Jiji akipoteza maisha wasithubutu kuomba kura kwenye kata hiyo kwa sababu kitendo cha serikali kushindwa kufanya uchunguzi na chama kukemea vitendo hivyo ni dharau kwao na wananchi wa eneo analotoka diwani huyo.

Walidai kuwa kitendo hicho kimefanywa dhahiri na watu wenye makusudi ya kutoa uhai wa meya huyo kwa kuwa tukio hilo ni la pili baada ya Machi 6, mwaka huu ambapo aliugua ghafla muda mfupi baada ya kurejea nyumbani akitokea ofisini na ikadaiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

“Waliofanya kitendo hicho ni wale ambao amewabana kwenye vitendo vya ufisadi na ubadhirifu wanaofanya hpo jiji .Tunataka tufahamishwe hatua zilizochukuliwa na serikali juu ya tukio la (jana)juzi la diwani wetu na Meya kupuliziwa vitu ofisini vinavyosadikiwa kuwa hewa chafu (sumu).

“Majiji ya upinzani manne yanayoongzwa na upinzani yako salama kati ya sitana kote huko hakuna mamboa kama haya.Ni mawili tu yanaongozwa na CCM je, hapa jiji la Mwanza kuna nini hadi aanadmwe na vitendo viovu vya aina hii? Tunataka uchunguzi kujua nani amepulizia hewa hiyo ya sumu.” Alisema Prudence Gabriel.

Aliongeza kuwa watumishi waliokaa kwenye halmashauri hiyo ya jiji kwa miaka 30 ni wahusika kutokana na kutuhumiwa kwenye ufisadi na baada ya kudhibitiwa wameamua kumhujumu meya aisitimize wajibu wake wa kutetea na kulinda maslahi ya wananchi wa Mwanza.
Mwingine Patrice Bulakali ambaye alidai kuwa kama tatizo ni umeya basi ajiuzulu awachie wachague wanayemtaka ili diwani wao huyo arejee kuwatumikia kwa sababu walimchagua awatumikie na kuhoji kwa nini watumishi wanahumu kwenye ofisi yake wasibadilishwe kutokana na tukio la kwanza nab ado wanaendelea kufanya kazi kwenye ofisi hiyo na hao watakiwa wanafahamu njambo hilo.

Akijibu madai na malalamiko ya wana CCM hao Kaimu Katibu wa CCM wa Wilaya Idd Mkoa alisema “ Hayo mnayopigia kelele na kulalamikia tumeyapokea na yaliyotokea jana chama tunataarifa nayo.Yawezekana ikawa sumu kwa mujibu wa maelezo yake au la na hijulikani nani kaipulizia maan walikuwa kwenye kamati ya kikao cha kamati ya fedha.”
Alisema wawe na subira kwa kuwa jambo hilo wameliachia vyombo vya usalama vifanye kazi yake kwani Mkemia wa serikali alifika kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi huku polisi nao wakifanya kazi yao ya kuchunguza tuhuma hizo.

“ Wakati haya yanafanyika tuwe watulivu vyombo vy uslma vifanye kazi yake baadaye tutapata majibu ya kitalaamu ya uchunguzi huo mara baada ya mkemia kufanyia uchunguzi sampuli aliyochukuwa na ikibainika kuwa ni sumu wahusika watachuliwa hatua.” Alieleza Mkowa.

Hata hivyo Mohamed Zabron alipinga kauli hiyo Mkowa akidai anashangaa wilaya kudai inafutailia tukio hilo la juzi wakati lile la awali hakuna hatua zimechukuliwa hadi sasa abapo alihoji chama kimechukua hatrua ga
Mkowa alieleza kuwa tukio la Machi halikutolewa taarifa rasmi ofisini na hata mwathirika mwenyewe hakuwa anafahamu kuwa kilikuwa kitu gani hadi anapelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

“ Hata yeye mwenyewe binafsi hakuwa anafahamu ni nini bali alikuja kugundua baadaye .Kwa hili amechukuliwa maelezo ndiyo maana tunawaomba muwe na subira tuviachie vyombo husika kwa ni majibu yetu hayapaswi kuingilia uchunguzi tunaweza kuvuruga hata ushahidi,”alidai kaimuj katibu huyo

Aidha , Katibu Mwenezi Mustafa Baningwa aliwaeleza wana CCM hao kuwa hawajalala juu ya tukio hilo bado wanafanya kazi kwa kushirikiana na vyombo husika na hawatakubali jambo hilo liishe kimya kimya bila umma kufahamu hatima yake na kwa vile ni mambo ya kitaalamu hawataki kuyachukulia kwa wepesi na kutoa majibu rahisi.

“ CCM hatuna vyombo vya uchunguzi bali wapo wataalamu ambao ni mkemia na wanalifanyia kazi hili ma liko katika eneo sahihi pamoja na jeshi la polisi kwa upande mwingine. Tunapaswa tuwachie nafasi ya kuchunguza na kisha watupe majibu,” alisema Baningwa

Machi 6, mwaka huu Bwire aliugua ghafla muda mfupoi baada ya kurejea nyumbani akitokea ofisini na hHali hiyo ilisababishwa alazwe katika Hospitali binafsi ya Uhuru na baadaye katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bungando kwa uchunguzi na matibabu hata hivyo Machi 7, mwaka huu familia Kwatibu yake iliamua kumhamishia katika hospitali moja iliyopo Naironi Kenya ambapo alifanyiwa vipimo na kubainika kuwa alivuta kiwango kikubwa cha sumu na kulazimika kulazwa .

Juzi akiwa na naibu wake na watendaji wengine wa Halmashauri ya Jiji walitembelea Kata za Mirongo na Mabatini ondogo (machinga) ya Community Centre Mirongo na baadaye Sinai katika Kata ya Mabatini na kurejea ofisini kwa ajili ya kukutana na kamati ya fedha.

Ilidaiwa kuwa majira ya saa 4:00 asubuhi kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea maeneo ya wafanyabiashara hao alikutana na kamati ya fedha na uongozi na aliporudi mchana akaomba akajisaidie haja ndogo ofisini kwake ndipo akkutana na dhahama hiyo.

Bwire alinukuliwa akisema kuwa abaada ya ziara aliwaomba wajumbe akajisaidie haja ndogo alipoingia ndani ya ofisi yake ndipo akakumbana na hewa nzito ikiambatana harufu kali na hivyo akalazimika kuwaita Mkurugenzi wa Jiji Adam Mgoyi, Naibu Meya Bhiku Kotecha , Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula ambao walifika na kushuhudia hali hiyo.
Habari ambazo hazijathibitshwa zinasema kuwa watumishi wawili wa ofisi yake Katibu muhtasi Glads Chiduo pamoja na Selestin Mutobesya walichukulia na polisi kwa mahojiano kabla ya kuachiwa hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alipogiwa simu na jana na gazeti hili kupata ufafanuzi wa kuhojiwa kwa watumishi hao iliita bila majibu.


No comments:

Post a Comment