BENKI ya Diamond Trust Tanzania (DTBT) imeanzisha kampeni maalum kupitia mitandao ya kijamii ambayo inalenga kutoa uelewa juu ya huduma wanazotoa kwa wateja na wadau mbalimbali. Mbali na hayo kampeni hiyo iliyopewa jina la 'miaka 70 jiunge nasi ushinde' imedhamiria kuwapa wadau wake zawadi mbalimbali hususani wanaowafuatilia kupitia mitandao ya kijamii ukiwemo Facebook.
Picha: MKUU wa Kitengo cha ICT kutoka Benki ya Diamond Trust Tanzania,Stella Mosha (kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa washindi wa kampeni yao ya 'miaka 70 jiunge nasi ushinde',Said Mpanju kutoka KIBAHA mkoani Pwani,mwishoni mwa wiki.Picha na DTBT 9( Na Mpiga Picha Wetu)
Hayo yalibainishwa Jana kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na benki hiyo huku ikisisitiza zawadi nyingi zitaenda kwa watakaokuwa wanajibu vema maswali kupitia mitandao hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo maswali mengi yatakuwa katika ukurasa wa benki wa,www.Facebook.com/DTB Tanzania.
"Miongoni mwa zawadi hizo in jezi za michezo,tiketi za sinema,vocha za manunuzi,Samsung Galaxy J7,simu za kisasa na kompyuta mpakato,"ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kampeni hiyo ni muendelezo wa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 70 ya DTBT kutoa huduma nchini ambayo imekuwa na mafanikio makubwa.
"DTB Tanzania imejizatiti kikamilifu kuwafikishia wateja wetu wa thamani huduma bora ikiwemo kupitia majukwaa haya ya kidigitali," alibainisha MKUU wa Kitengo cha Huduma na Masoko DTBT,Sylivester Bahati. Aliongeza kuwa,mitandao ya kijamii itawasaidia kuwasiliana moja kwa moja na wadau wao wakiwemo wateja ili kupeana tasrifa juu ya Yale yanayojiri katika jamii na ndani ya banki. "Pia tumejipanga kuongeza ukaribu zaidi na wadau wetu.Kwani tumejipanga kuwapa huduma bora zaidi," alisema.

No comments:
Post a Comment