* YAUNGANA NA ORODHA YA MIJI MASHUHURI AFRIKA KUTOA HUDUMA YA
UBER
Dar es Salaam, Juni 2016. Leo, Dar es Salaam inakuwa mji wa
475 kujiunga na mtandao unaokuwa wa Uber duniani. Kwa uzinduzi wa Uber, jukwaa
la ubunifu wa kiteknolojia, Dar es Salaam inaungana na orodha ya vituo maarufu
vya usafiri barani Afrika.
Kufuatia mafanikio ya Uber katika nchi nyingi, Uber
inayo furaha kuzindua jukwa la ushirika la abiria kwa watu wa Dar es Salaam.
Uber Dar es Salaam
Jukwaa la mtandao wa ubunifu la Uber, huwaunganisha madereva
na wasafiri kwa muda muafaka, kwa kubonyeza tu kitufe. Au ukiwa unatoka na
marafiki kwenda mjini kibiashara, au kuangalia vivutio vya kitalii, Uber hutoa
njia rahisi yenye unafuu kufika kila mahali.
Dar es Salaam Jiji linalokua kwa kasi kibiashara, linafanya
iwe ni mahali sahihi kwa Uber. Taarifa za Benki ya Dunia zinasema kwamba Pato
halisi la Tanzania (GDP) linakadiriwa kuwa 6.8% kwa mwaka 2017 na nchi imeweza
kuhimili mfumuko wa bei. Biashara zinakua kwa kasi katika sekta za usafiri,
ujenzi na fedha.
Meneja wa Uber Kusini
mwa Sahara, Alon Lits anasema:
“Tunajivunia kuzindua Uber nchini Tanzania katika muda ambao
uchumi wake unakua. Wakati miundo mbinu ya Dar es Salaam ikiwezeshwa kuwa ya
viwanda, hivyo huongezeka kwa mahitaji ya usafiri nafuu, rahisi na wa
kuaminika.”
Akaongeza, “Tumeweka viwango vya kuunganisha watu katika
usafiri wenye kiwango cha juu duniani, kusafirisha mamilioni ya watu duniani
kote kila siku kupitia huduma zetu za usafiri nafuu na za kuaminika kwa
kubonyeza kitufe tu. Huduma zetu zinaenda sambamba na aina za usafiri uliopo,
hivyo wote tunaweza kufanya kazi pamoja kupunguza foleni barabarani na
kuboresha mazingira ya usafiri katika jiji.
Kwanini Uber?
Uber husaidia watu kupata usafiri kwa kubonyeza tu
kitufe-hakuna kusubiri barabarani au kutembea maeneo jirani usiyoyajua kwa
ajili kutafuta basi. Ni njia bora na karibu zaidi kupata usafiri salama, nafuu
na wa kuaminika.
Kabla ya kuingia
ndani ya gari
Hakuna haja kusimamisha gari mtaani au kuwa nje kusubiri
usafiri. Kwa usalama zaidi utaweza kutumia App ya Uber mahali ulipo ukisubiri
gari ifike. Hii ikimaanisha hakuna haja ya kusimama barabarani kusubiri taksi
au kuhangaika kutafuta kituo cha basi kilicho karibu muda wa usiku.
Safari hazina kificho. Mara dereva anapokubali ombia lako,
unaona jina lake la kwanza, picha na namba ya gari yake. Pia unaweza kuangalia
kama kuna abiria wengine waliofurahia huduma yake. Kwa kuongezea, dereva
anaweza kuona jina lako la kwanza na alama ulizompa. Unaweza kuwasiliana na
dereva, naye pia akawasiliana nawe-kupitia hii App kama kuna mkanganyiko wowote
kuhusu muda wa kukuchukua.
Wakati wa Safari
Julisha mahali ulipo. Unaweza kuwajulisha ndugu na
marafiki zako kwa furaha zaidi juu ya mipango ya safari yako kwa urahisi, ikiwa
ni pamoja na mahali ulipo, na muda unaotarajia kuwasili. Watapokea linki ambapo
wataweza kuona muda kamili, jina na picha ya dereva, gari lake na mahali ulipo
katika ramani hadi utakapowasili na wanaweza kufanya haya yote bila haja ya
kupakua App ya Uber wao wenyewe.
Baada ya Safari
Fanya mrejesho na toa alama kila baada ya safari. Baada
ya kila safari, wewe na dereva wako mnahitaji kupeana alama na kufanya
mrejesho. Timu yetu ya usalama hupitia taarifa hizi na kufanya uchunguzi juu ya
kila jambo.
Msaada masaa 24 kwa wiki. Endapo jambo litatokea
ndani ya gari, kama ni ajali ya barabarani au kutoelewana kati yako na dereva,
mfanyakazi wetu wa huduma kwa wateja yupo tayari kukusaidia kwa suala lolote
masaa 24 kwa wiki.
Msaada wa Haraka. Tuna timu mahiri inayoshughulika na
matukio kujibu suala lolote linalohitaji ufumbuzi wa haraka. Tukipokea
taarifa kuwa dereva au abiria amesababisha tukio la hatari au hayupo
njia sahihi, tunafunga akaunti zao na kumzuia asiweze tena kuingia katika
jukwaa la Uber wakati tukifanya uchunguzi.
Nyuma ya Pazia
Muda wote kwenye ramani. Kukubali kuwajibika ni moja ya
mambo yanayofanya wasafiri kujisikia wako salama ndani ya Uber. Tunatumia
teknolojia ya mawasiliano ya GPS kuweka taarifa za mahali madereva wanakotakiwa
kwenda wakati wa safari, ili kutuwezesha kuthibitisha njia zinazotumika ni
bora, kitu kichanachojenga uwajibikaji na ushawishi mkubwa kwa utendaji mzuri.
Utendaji na mamlaka za sheria. Endapo mamlaka za
kisheria zinatupa taratibu za kisheria, tunatafanya kazi kutafuta vielelezo,
mfano kwa kutoa taarifa za safari. Hata hivyo uwazi na uwajibikaji upo katikati
ya mafanikio ya Uber.
Upimwaji wa madereva. Madereva wote lazma awapitie
mchakato wa upimwaji kabla ya kuanza kutumia App ya Uber
Alon Lits aliongeza:
“Uber ni sehemu ya mageuzi makubwa duniani katika Nyanja ya
usafirishaji. Dar es Salaam ipo juu, inazizima, mji unaokuwa ukiwa na vijana
mahiri wenye nguvu ya kufanya kazi ambao wapo tayari kutukaribisha na kusapoti
huduma yetu. Pamoja, kwa ushirikiano na mipango ya usafiri iliyopo jijini Dar
es Salaam tunaweza kubadilisha sura ya usaifiri wa mjini kunufaisha abiria.
Tuna furaha isiyo na kifani kwa uzinduzi huu.”
Uber inasherehekea uzinduzi mjini Dar es Salaam kwa kutoa
huduma ya bure ya usafiri. Tanzania wanaweza kujaribu huduma mpya kwa kupata
huduma ya bure kwa kuingia kwenye App ya Uber. .
MAKUBALIANO (vigezo kwa usafiri wa bure)
Ni lazima upakue App ya Uber na weka kificho cha promosheni MoveTanzania
ili upokee usafiri wa bure
Usafiri wa bure utapatikana kutoka Alhamisi Juni 16 saa 6
mchana mpaka Jumapili Juni 19 katikati ya usiku.
Watumiaji watapata usafiri wa bure kwa safari sita tu na
kila safari isizidi kiasi cha shs 12,000
Usafiri wa bure utapatikana tu kwa safari zinazoanzia na
kuishia maeneo ya Dar es Salaam yaliyopangwa.
- Mwisho -
Kuhusu Uber
Uber ni kampuni ya teknolojia inayowaunganisha wasafiri na
madereva kwa kiasi cha kubonyeza kitufe. Hupatikana kwenye miji 475 katika nchi
73, jukwaa la Uber hujumuisha jinsi dunia inavyokwenda. Malengo ya Aber ni
kubadilisha mtazamo wa watu jinsi wanavyokwenda duniani, kufanya kazi na
kuishi. Inajihusisha kubadilisha jinsi watu wanavyoungana na familia zao, hivyo
huleta uaminifu na ukaribu kwa kutoa nafasi katika mipango ya usafiri.
No comments:
Post a Comment