Na MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imesema itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za
Miko na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo wakati akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalum. Mhe. Sophia Mwakagenda aliyetaka kujua utayari wa
Serikali katika kukubali ombi la Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe,
Mkoani Mbeya na kuongeza fedha katika Bajeti ya mwak 2016/2017.
Mhe.
Jafo amesema kwamba, Halmashauri ya Rungwe iliandaaa makisio ya bajeti
ya Shilingi bilioni 7.9 kwa ajili ya matenegenzo ya barabara katika
bajeti ya mwaka 2016/17, hata hivyo kutokana na ukomo wa bajreti fedha
zilizoidhinishwa ni shilingi milioni 920 ambazzo zitatumika kwa ajili ya
matenegenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja.
"Katika
mwaka wa fedha wa 2015/16, Halmashauri hiyo ilitengewa shilingi milioni
870 na tayari Serikali imeshapeleka milioni 157.9", alisema Mhe. Jafo.
Aliongeza
kuwa, fedha za Mfuko wa Barabara katika bajeti ya mwaka wa fedha wa
2016/17 ni shilingi bilioni 247.5 ambazo endapo zingegawanywa sawa kwa
Halmashauri zote 181 zilizopo, kila Halmashauri ingekuwa na bajeti ya
shilingi bilioni 1.3.
Amefafanua
kuwa mara zote mahitaji yamekuwa ni makubwa kuliko uwezo wa rasilimali
fedha kukidhi mahitaji hayo ndiyo maana Serikali inaweka vipaumbele ili
kutekeleza mambo machache kwanza kulingana na uwezo uliopo kibajeti.
"Serikali itaendelea kuongeza bajeti kwa ajili ya barabara kadri uwezo wa kifedha utakavyoongezeka", alisema Mhe. Jafo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment