Mwezi Aprili mwaka huu umekuwa mwezi wenye joto zaidi katika historia ya dunia, limesema Shirika la Hali ya Hewa duniani WMO katika ripoti yake ya jana (Jumamosi).
Taarifa iliyotolewa la WMO inaonyesha kwamba wastani ya halijoto ya mwezi Aprili imezidi wastani ya karne ya 20 kwa nyuzi 1.1 ya Selisiasi.
Clare Nullis ni msemaji wa WMO na amesema, "joto tuliloshuhudia mwaka 2015 liligonga vichwa vya habari wakati ule, na tulikuwa na wasiwasi mkubwa." Ameongeza kuwa Joto la mwaka 2016 linaifanya mwaka 2015 kuonekana afadhali.
Amesema sababu ya kwanza ya kuweko joto kubwa zaidi mwaka huu, ni ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi yaliyosababishwa na mikono ya binadamu.”
Kwa msingi huo Bi Nullis amesisitizia umuhimu wa kuchukua hatua mara moja za kutekeleza makubaliano ya Paris ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.
Miji ya Afrika Mashariki kama vile Dar es Salaam, Mombasa na Nairobi imekuwa ikishuhudia joto kali katika miezi ya hivi karibuni na hata katika baadhi ya maeneo kusababisha vifo.
No comments:
Post a Comment