Monday, April 25, 2016

NA HII NDIO NEMBO MPYA YA OLYMPIC TOKYO 2020

Na Mwandishi Wetu.
Waandaaji wa michezo ya Olimpik wamezindua nembo mpya ya michezo hiyo inayotarajiwa kufanyika jijini Tokyo nchini Japan mwaka 2020, mapema leo, wakiangalia rangi nyepesi ya bluu na nyeupe pamoja na dizaini ya kipekee.

Nembo hiy imebuniwa na mbunifu wa Japan, Asao Tokoro, inachanganya rangi tatu zinazokaribiana za bluu ikiwa na sura ya mstatili ikiwakilisha nchi, tamaduni mbalimbali pamoja na namna watu mbalimbali wanavyofikiri.

“nilibaki nashangaa niliposikia nembo yangu ndio imeshinda,” alisema Tokoro “nilitumia muda na jitihada nyingi katika nembo hiyo kama vile ni mtoto wangu”

nembo halisi iliyobuniwa na mbunifu wa Kijapan Kenjiro Sano ilitupiliwa mbali mwaka jana ikituhumiwa kwa kuibia kwani ilifanana nembo ya jumba la maonesho la nchini Ubelgiji.


No comments:

Post a Comment