Tuesday, April 05, 2016

DTB YAVUNA FAIDA YA SHILINGI BILIONI 27.3 MWAKA 2015

Diamond Trust Bank Tanzania, (DTB), imetangaza mafanikio makubwa katika matokeo ya biashara kwa mwaka 2015. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa DTB inakua kwa kasi ukilinganishwa na ukuaji katika sekta ya kibenki.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa faida kabla ya kodi mwaka 2015 ilikuwa shilingi bilioni 27.33 sawa na ongezeko la asilimia 36.03% ikilinganishwa na shilingi bilioni 20.1 mwaka 2014.

Akiba za wateja  zimekua kwa asilimia 26.8%  kutoka shilingi bilioni 570 mwaka 2014 hadi shilingi bilioni 737 mwaka 2015. Aidha, kulingana na ripoti za mabenki zilizotolewa kwa mwaka 2015, DTB ni benki ya sita kwa ukubwa wa amana za wateja nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa DTB, Ndg. Viju Cherian(Pichani Katikati) akizungumza na waandandishi wa habari, alisema kuwa rasilimali za benki ziliongezeka kwa asilimia 30.5% kufikia shilingi bilioni 900  mwaka 2015 kutoka shilingi bilioni 690 mwaka 2014.


Aliongeza kuwa “Rasilimali za benki zimekuwa zikiongezeka mwaka hadi mwaka kwa kiwango cha kati ya 26.4% na 36.4% kwa kipindi cha miaka minane hadi mwaka 2015. Benki imeendelea kuimarika katika nyanja zote kwa kipindi hicho huku ikiongeza mtaji wake kwa shilingi bilioni 12 mwaka 2012 na shilingi bilioni 30 mwaka 2015 kwa kuuza hisa stahiki kwa wanahisa wake.

Mikopo kwa wateja iliongezeka kwa asilimia 31.6% mwaka 2015 na kufikia shilingi bilioni 536 kutoka  shilingi bilioni 407 mwaka 2014. DTB pia imefanikiwa kudhibiti kiwango cha mikopo isiyolipika ndani ya asilimia 2% ikiwa ni kiwango cha chini kulinganishwa na kiwango cha sekta ya kibenki.

Ndg. Cherian aliongeza, “DTB pia ilishiriki katika shughuli za kijamii mwaka jana katika sekta za Afya, Elimu na Mazingira, ambapo zaidi ya shilingi milioni 200 zilitumika. Nia na lengo kuu ikiwa ni kuboresha maisha ya watanzania katika nyanja za elimu, afya na hata mazingiza safi na rafiki”.

DTB Tanzania ina matawi 25 nchini, ikiwa na matawi kumi na moja (11) jijini Dar es Salaam (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, barabara ya Nyerere, Msimbazi - Kariakoo, barbara ya Nelson Mandela , Upanga katika barabara ya umoja wa mataifa na katika makutano ya barabara ya Mirambo na mtaa wa Samora). Vile vile ina matawi katika miji ya Arusha (2), Mwanza (2) na katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora , Tanga na Zanzibar.

DTB Tanzania ni mshirika wa mtandao wa maendeleo ya kiuchumi wa Aga Khan - Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ambao ni sehemu ya mtandao wa maendeleo wa Aga Khan Development Network). DTB Kenya ni miongoni mwa wanahisa muhimu wa DTB Tanzania.

DTB Tanzania pia ni sehemu ya mtandao wa wa mabenki ya DTB Group yenye matawi zaidi ya 120 Afrika Mashariki katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi.



No comments:

Post a Comment