Friday, April 15, 2016
DIAMOND TRUST YAKABIDHI MADARASA MAWILI SHULE YA JITIHADA, KITUNDA
Bi Elizabeth Thomas, Mwakilishi kutoka ofisi ya Manispaa ya Ilala akipeana mkono na Bw. Viju Cherian, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Diamond Trust (DTB) wakati wa sherehe ya kukabidhi madarasa mawili yaliyojengwa na Benki hiyo katika shule ya msingi Jitihada leo, iliyopo katika Kata ya Kitunda. Bw. Viju aliahidi kutengeneza madawati kwaajili ya madarasa hayo na kumalizia jengo la utawala la shule hiyo. ( Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Diamond Trust (DTB), Bw. Viju Cherian akipokea ujumbe wa shukrani kutoka kwa mwakilishi wa Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas katika shughuli ya kukabidhi madarasa mawili shule ya msingi Jitihada mapema leo ambayo ujenzi wake umekamilika. Madarasa hayo yamejengwa na kufadhiliwa na Benki hiyo. Katikati ni Diwani wa kata ya Kitunda, Nice Gisunte. ( Na Mpiga Picha Wetu)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment