Mshambuliaji wa klabu ya Yanga ambao ni washindi wa pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara, Didier Kavumbago amesema kuwa hadi sasa hajui mustakabali wake katika timu hiyo kwani mkataba wake umeisha na hadi sasa haujaongezwa kitu ambacho kinamshangaza.
Kavumbago amesema anatoa nafasi kwa klabu yoyote itakayo muhitaji kwani anahisi kuwa Yanga hawamuhitaji tena wakati wao ndio waliomleta nchini.
“Niko tayari kwenda timu yoyote kama wako tayari kunisajili, mkataba wangu na Yanga umekwisha” alisema Kavumbago alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi. Alisema hawaelewi viongozi wa timu hiyo na kwamba ametoa fursa kwa timu yoyote itakayo muhitaji ataingia nayo mkataba
Kavumbago alisema hayo baada ya kumalizika kwa mechi baina ya Taifa Stars na Burundi katika kusherehekea miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo Burundi waliibuka na ushindi wa magoli 3 – 0, huku mashabiki wakijikuta wanaishangilia timu ya Burundi
Naye mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Tambwe amesema kuwa yeye yupo kimaslahi zaidi na kwamba yuko tayari kuchezea klabu yoyote itakayo muhitaji, ila kwa sharti kama watavunja mkataba wake na samba kwani bado mkataba wake haujaisha.
Alisema kuwa yeye amekuja kufanya kazi na timu itakayomchukua ndio timu atakayokuwa na mapenzi nayo.
TAFADHALI SHUKA CHINI UTOE MAONI YAKO. . .
No comments:
Post a Comment