Thursday, March 31, 2016

WABUNGE WATATU WABURUZWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA

Screen Shot 2016-03-31 at 2.13.21 PMTaasisi ya kuzuia na kupambana  rushwa tanzania  (TAKUKURU ) imewafikisha mahakamani wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM),kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya  rushwa.

Wabunge hao  ambao pia ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya hesabu za serikali za mitaa ni pamoja na mshitakiwa namba moja Sadick Murad wa jimbo la Mvomero Morogoro, mshitakiwa namba mbili  Kangi Lugora wa jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda na mshitakiwa namba tatu Victor Mwambalaswa wa jimbo la Lupa mkoani Mbeya.
Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mahela Ndimbo mbele ya Hakimu Mkazi mkuu wa mahakama ya Kisutu, Thomas Simba amesema washtakiwa hao wakiwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa (LAAC) walimuomba rushwa  mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoani morogoro ya shilingi millioni thelathini ili waweze kumsaidia kupata hati safi ya mahesabu kwa mwaka 2015/16.
Tukio hilo linadaiwa  kutokea machi 15 mwaka huu majira ya saa 2 hadi saa 4 katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Washitakiwa wote watatu wamekana mashitaka, na hakimu ameahirisha kesi hiyo hadi April kumi na nne mwaka huu, huku akiwataka TAKUKURU wahakikishe wanakamilisha ushahidi wao kwa haraka.
Aidha dhamana ilikuwa wazi kwa watuhumiwa wote watatu,ambapo kila mmoja alitakiwa awe  na mdhamini mmoja mwenye vitambulisho vinavyotambulika, pamoja na dhamana ya fedha taslim shilingi  million tano.


20160331065736



No comments:

Post a Comment