Thursday, March 31, 2016

REA:HATUTEGEMEI MSAADA WA MCC


Wakala wa Nishati Vijijini (REA)imesema  haitaathirika na kusitishwa kwa msaada wa mamilioni ya fedha uliokuwa utolewe na Shirika la Maendeleo la Milenia (MCC), hivyo mradi huo utaendelea kama kawaida.
Hayo yamebainishwa  leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu REA,Lutengano Mwakahesya, alipokuwa akitoa tathmini ya upelekaji umeme vijijini kwa awamu ya Pili.
"REA hatujawahi kupata fedha za MCC tangu tuanze  kupeleka umeme vijijini, bali mradi huu unafadhiliwa na serikali kwa asilimia 90,wananchi wasiwe na wasiwasi, kwani shughuli za upelekaji umeme vijijini itaendelea kama kawaida kwa kuwa mradi huo unategemea fedha za Serikali kwa kipinchi chote na asilimia 10 ndiyo inachangiwa na wahisani"anaeleza.
Amesema MCC ilikuwa na ofisi zake nchini, lakini walikuwa wanatekeleza miradi yao wenyewe, hivyo kwa upande wa REA hatujaathirika kama  inavyodaiwa, kwani hatujawahi kupata fedha hizo tangu tuanze kupeleka  umeme vijijini..Pia amesema wameweza kusambaza umeme kwa vijiji 5,200 tangu waanze kazi hiyo na  wanakusudia kuendelea zaidi katika kutoa huduma zaidi kwa wananchi,Mwakahesya anasema kukamilika kwa mradi huu wa upelekaji umeme vijijini awamu ya pili ambayo inaisha Juni 30, mwaka huu kiasi cha sh. bilioni 881 zimetumika.Anaongeza kuwa bado fedha zinazotolewa hazitoshi kutokana na kuwepo kwa uhitaji zaidi ili kufikia wateja wengi zaidi.
Hata hivyo amesema kuwa  licha ya Serikali kwa kutumia fedha nyingi kusambaza umeme vijijini, bado mwamko wa wananachi kuunganishiwa umeme ni mdogo. Aliwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kupata  maendeleo kwa haraka na wanatarajia kupata fedha zaidi kwa Serikali ili kufikia vijiji na mikoa yote Tanzania 

No comments:

Post a Comment