Wednesday, March 09, 2016

MCHUMBA WA MTOTO WA BOBBY BROWN ALIJARIBU KUOKOA MAISHA

Aliyekuwa boyfriend wa Bobbi Kristina Brown, Nick Gordon alijaribu kuokoa maisha yake baada ya kumkuta binti huyo kwenye sinki la kuogea akiwa haijtambui, wanasheria wake wamesema. Wanasheria waliwataka waendesha mashtaka kuacha kuzusha kifo cha mtoto wa marehemu Whitney Huston ni matokeo ya kutokuelewana kulikosababishwa na Gordon.

Kwa mujibu wa Sky News, wanasheria hao wanadai kuwa Gordon amelengwa kimakosa katika kesi ya uchunguzi ya kifo cha Kristina kilichotokea mwaka 2015. Wanasheria Joe Habachy na Jose Baez wanadai: “ukweli ni kwamba Nick alijaribu kumsaidia Bobbi Kristina kuokoa maisha yake. Na ukweli ni kwamba Nick ametoa ushirikiano katika kesi hiyo tokea siku ya kwanza”

“Mwendesha mashtaka kutoka katika ofisi ya Wilaya ya Fulton amekuwa akijaribu kujenga hoja ya kuwa Nick amehusika na kifo cha Bobbi Kristina pamoja na kwamba ushahidi wote unaonesha kifo hicho ni matokeo ya ajali iliyomkuta binti huyo” waliongeza wanasheria hao katika taarifa iliyotolewa.

Wanaeleza kuwa “ ukweli ni kwamba hakuna aliyempenda Bobbi Kristina zaidi ya Nick na hakuna aliyeguswa na kifo cha Bobbi Kristina kama alivyoguswa Nick” Gordon and Bobbi Kristina walijitambulisha kama mke na mume lakini baba wa msichana huyo, Bobby Brown alidai hawakuwahi kufunga ndoa kisheria.

Wahifadhi wa miliki ya mali ya Bobbi Kristina wamefungua kesi wakimtuhumu Gordon kwa kusababisha kifo ili kuiba hela kutoka kwenye akaunti wakati akiwa mahututi kabla ya kupoteza maisha mwaka yana mwezi julai.

Goron amedai kuzuiliwa kumuona mpenzi wake katika kipindi cha miezi sita alipokuwa amelazwa mahututi. Waendesha mashtaka wamesema kuwa uchunguzi wa kifo cha Bobbi Kristina unaendelea lakini hawakutaja majina ya wanaolengwa katika uchunguzi huo.

Bobbi Kristina alikuwa na miaka 22 alipozama kwenye sinki la kuogea nyumbani kwake huko Atlanta, Georgia, nchini Marekani mwaka jana.

Matokeo ya uchunguzi yaliyotangazwa wiki iliyopita haukuonesha kama kifo chake ni matokeo ya ajali au tendo la kukusudia kama kuuawa au kujiua. Madaktari waliofanya uchunguzi hawakusema lolote zaidi ya kusema sababu za kifo chake hazijafahamika. Kifo chake kimetokea miaka mitatu baada ya mama yake kufariki katika sinki la kuogea katika hoteli iliyoko Beverly Hills akiwa na miaka 48.





No comments:

Post a Comment