Tuesday, February 02, 2016
WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUHAKIKI SILAHA ZAO KWA WAKATI
Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha,
Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa njia halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na kuzilipia kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria inavyoagiza.
Hayo ya mesemwa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwaajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili ,na kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha, itasimamishwa kwaajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi Kamanda amesema utaratibu huu huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi kwaajili ya kuhakiki silaha ,ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya serikali ,amewataka watu wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama inavyotakiwa, nawakumbuke sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa ,na kama mtu akiitumia ndivyosivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia sheria iliyowekwa.
Ameongeza kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao zipo tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria, amesema kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti yakufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa umiliki, amesema kuwa ukitoka nje ya hayo masharti huna sifa ya kumiliki silaha.
Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi .
Amehitimisha kwa kusema kuwa kila , mtu amnayetaka kumiliki silaha, kamati za ulinzi na usalama kuanzia kwenye kata ,Wilaya, Mkoa wakamuidhinisha kuwa na silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake, Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment