Thursday, February 18, 2016

WAZIRI MKUU : WEKEZENI KATIKA SEKTA YA MICHEZO


Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipowasili katika Uwanja wa Ndani wa Michezo kabla ya kikao baina yake na wadau na viongozi wa vyama vya michezo jana jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akielekeza jambo kuhusu mradi wa kuendeleza Uwanja wa Ndani wa michezo jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipowasili katika Uwanjwa wa Ndani wa Michezo kabla ya kikao baina yake na wadau na viongozi wa vyama vya michezo jana jijini Dar es Salaam.




No comments:

Post a Comment