Na MAELEZO.
Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Feminist and Youth
Change Organization (TAFEYOCO) limemuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuanzisha utaratibu wa kukutana na vijana ili kujadiliana
mambo mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bw. Elvis
Makumbo alipokuwa akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam katika
mkutano uliyolenga kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika siku mia moja za uongozi wake.
“Vijana kwa sasa katika taifa ni wengi na ndiyo wenye uwezo
wa kuleta maendeleo katika nchi na nguvu kazi ya Taifa na wanachangamoto nyingi
hivyo Mheshimiwa Rais akijaribu kukutana nao nakuwasikiliza
matatizo yao itasaidia kuleta mafanikio katika nchi na kujua nini kifanyike
kuleta maendeleo katika Taifa,” alisema Bw. Makumbo.
Ameleza kuwa, Mheshimiwa Rais ameonyesha moyo wadhati wa
kuwatumikia wananchi kwa kuwawajibisha watu wote walionekana wakitumia vibaya
madaraka yao na kufanya ubadhirifu wa pesa za umma kinyume na taratibu za
kiutumishi wa umma.
Mbali na hayo Bw.Makumbo amemuomba mheshimiwa Rais kufikiria
kuanzisha mfumo au taasisi itakayohakiki mali za mtumishi wa umma na kuhoji ni
namna gani mali hizo amezipata ili kupunguza wimbi la watumishi wa umma wanao
tumia fedha za serikali vibaya kwa kujinufaisha wenyewe huku wakijiwekea
utajiri mkubwa usiyolingana na kipato chao.
Mwenyekiti huyo aliendelea kumwomba Mheshimiwa Rais kuzidi
kuzingozea nguvu taasisi za Serikali ili kuzijengea uwezo mkubwa wa kiutendaji
mfano wa Taasisi hizo ni TAKUKURU na nyinginezo zinazosimamia mambo mbalimbali
Yenye tija kwa Taifa.
Shirika hilo limesema Kauli Mbiu ya Mheshimiwa Rais ya Hapa
Kazi Tu imeongeza hari kubwa ya utendaji kwa wananchi kwa kuwahimiza kuwajibika
ikiwemo kwa watu wa sekta binafsi na taasisi za umma.
No comments:
Post a Comment