Wednesday, February 03, 2016

WAMERUDIA TENA...WAKENYA WATOKA NA UZUSHI MWINGINE KUHUSU MAGUFULI

Katika mtandao wa The Spectator wa nchini Kenya , kuna habari iliyoandikwa na kuwekwa tarehe 31/01/2016 yenye kichwa cha habari (PICHANI CHINI) “All Ministers & Public Officials must use Probox or Vitz” orders Magufuli (ikimaanisha ‘Mawaziri wote na Watumishi wa Uma waanze kutumia magari kama Probox au Vits’ aamrisha Magufuli)

Taarifa hii imesambaa katika mitandao ya jamii. Lakini swali kubwa ni lini Rais Magufuli alisema hayo na mbona sisi Watanzania ambao ndio wahusika hatuna habari na taarifa hiyo?

Nahisi wenzetu wanafurahia kuendeleza uzushi usio na msingi wowote. Tafadhali idara husika chukueni hatua haraka.




No comments:

Post a Comment