Friday, February 05, 2016

UBALOZI WA INDIA NCHINI WAONGELEA SUALA LA MTANZANIA KUDHALILISHWA


                                     KWA UFUPI HAYA NDIO WALIYOSEMA

Waziri wa Uhusiano wa Nje wa India,Bi. Shushma Swarah alisema jana “tumeumizwa sana kwa kitendo cha aibu”. Naye Katibu wa Wizara hiyo, Bw. Amar Sinha aliongea na Ubalozi wa Tanzania ulioko New Delhi, India akilaani tukio hilo.

Wizara hiyo imekuwa ikifuatilia kwa karibu sana kwa kushirikiana na uongozi wa jimbo la Karnataka. Katika ripoti yake, Kamishna wa Polisi wa Bengaluru amehakikisha hatua kali zinachukuliwa kuzuia matukio kama hayo siku zijazo.
Serikali ya India imehakikisha kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kuhusiana na suala hilo na adhabu kali zitatolewa kwa wote waliohusika na shambulizi hilo. Kesi ya jinai imefunguliwa na watuhumiwa watano wameshakamatwa.

Serikali ya India imehakikisha kuwa hatua kali zinachukuliwa kuhakikishia usalama wanafunzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika waliopo India

Tarehe 5 februari, timu ya pamoja inayohusisha Ubalozi wa Tanzania nchini India na maofisa wa ngazi ya juu wametembelea mji wa Bengaluru na wataongea na wanafunzi kutoka Afrika ili kuwahakikishia usalama wao na maisha yao

No comments:

Post a Comment