Wednesday, February 03, 2016

SERIKALI KUTUMIA MILLIONI 300 KUJENGA BARABARA RUKWA










Picha Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na MAELEZO


(Na MAELEZO )
Serikali katika mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi million 300 kwa ajili matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe katika Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili kufanya Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.

Akijibu swali la Mhe.Desdelius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini (CCM) liliouliza ni lini Serikali itaitikia kilio hiki cha wananchi wanaopata shida kwa Barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha mwaka,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani amesema Serikali kupitia Wizara yake imesikia kilio cha wananchi wa Wilaya ya Nkasi na inaendelea kutoa fedha za matengenezo ya Barabara ya Kitosi-wampembe.

“ Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitoa jumla ya Shillimgi Millioni 500 ili kufanya matengenezo ya Barabara ya Kitosi-Wampembe ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka” Alisema Mhe Ngonyani.

Aidha ,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitenga jumla ya Shillingi Millioni 45 na Shillingi Millioni 60 zimetengwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 kwa ajili ya matengenezo ya aina mbalimbali ya barabara ya Nkana-Kala kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili kuhakikisha inapitika kwa kipindi chote cha mwaka.

Ukarabati wa barabara ya Kitosi-Wampembe yenye urefu wa kilomita 67 na Barabara ya Nkana –kala yenye urefu wa kilometa 68 uko chini ya Mfuko wa Barabara ikisimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Barabara zote hizi ziko chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambayo inawajibika kuwezesha Barabara zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka.



No comments:

Post a Comment