Na Agnes Alcardo
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ney wa Mitego (Ney the true boy) ameibuka tena na kudai siku zote huandika vitu baada ya kufanya uchunguzi wa hali ya juu.
Ney alitoa kauli hiyo baada ya mahojiano na mwandishi mmoja wa habari, juu ya habari zilizoenea mitandaoni mapema wiki hii kuhusu kuharibika kwa mimba ya msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu.
Wema ambaye alidai kupewa mimba na mpenzi wake Idriss Sultan, hivi karibuni habari zilienea katika mitandao ya kijamii ikiwemo Istagram, ambapo mshindi huyo wa mashindano ya Big Brother (BBA) 2014 aliandika katika ukurasa wake kuhusiana na mimba hiyo ya mpenzi wake kuharibika.
Katika ujumbe wake kupitia ukurasa huo ulioandikwa kwa lugha ya kingereza ulisomeka hivi ; "Kwa mapacha wangu niliowatarajia, mmekuja haraka sana kwenye maisha yetu na kuondoka, sikupata nafasi ya kukutana nanyi ila kuna mengi nataka kusema, nina mawazo mengi kichwani yanatosha kunifanya nichanganyikiwe.
"Pamoja na kwamba mliishi kwa muda mfupi wa wiki 13 nina wapenda sana, natamani ningewabeba na kuwashika...Naomba tupate nafasi ya kukutana katika maisha mengine, Mungu amewaleta na kuwachukua kwa mpango wake na hatuwezi kulalamika bali kuomba kuwa hayo yote ni kwa mpango wenye nia njema kwetu."
Ujumbe huo uliendelea; " Tumejifunza kwa uchungu lakini hatutoacha kuendelea kujaribu tena na tena na tutakapojaliwa kupata kaka na dada zenu tutakuwa tayari kwa ajili yao." Ujumbe huo umezua sintofahamu kwa watu wengi, huku wengine wakiandika mitandaoni kuwa suala la mlimbwende huyo ambaye ni Miss Tanzania 2006, hakuwa na ujauzito bali ni njia ya kujitafutia umaarufu 'kiki'.
Baada ya Ney wa Mitego kuhojiwa alidai kwa kile alichoamini kuwa, siku zote amekuwa akiongea ukweli na pengine hata wimbo wake mpya alioutoa hivi karibuni wa 'Shika adabu yako' kuwa asilimia kubwa ulikuwa na ukweli. "Baada ya Wema kuja na drama mpya na jamaa yake, sasa ni zamu ya mtu mwenye dimpoz nyingi duniani 'kuprove' kama kweli jogoo wake ana wika au ndiyo anakula tu mahindi na mchele" alisema Ney
Hata hivyo Ney wa Mitego alisema, baada ya kutoa ngoma hiyo hivi sasa anaandaa nyingine, ambayo itakuwa ikiwakosoa wabunge na mawaziri pekee na tayari juzi jioni alimaliza kuandika mistari inayomuhusu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye.
No comments:
Post a Comment