Katika hali ya kusikitisha Idrisa Sultani aliandika mapema leo alfajiri kwenye wall yake ya instagram (Pichani Juu) kwa huzuni na masikitiko makubwa baada ya kupoteza watoto mapacha. Tetesi zilianza kuzunguka katika mitandao ya jamii, kuhusu ujauzito wa Wema Sepetu (ambaye ndie aliyekuwa mjamzito wa watoto hao) kuharibika.
Tafrisi
“Kwa mapacha wangu
niliowatarajia,
Mmekuja haraka sana
kwenye maisha yetu, haraka sana na kuondoka. Sikupata nafasi ya kukutana nanyi.
Kuna mengi nataka kusema. Nna mawazo mengi kichwani mwangu, yanatosha kunifanya
nichanganyikiwe. Pamoja na kwamba mliishi kwa muda mfupi wa wiki 13,
ninawapenda sana. Natamani ningewabeba, natamani kuwashika. Naomba tupate
nafasi ya kukutana katika maisha mengine. Mungu amewaleta na kuwachukua kwa
mpango wake na hatuwezi kulalamika bali kuomba kuwa hayo yote ni kwa mpango
wenye nia njema kwetu. Tumejufunza kwa uchungu lakini hatutoacha kuendelea
kujaribu tena na tena na nnaapa tutakapojaliwa kupata kaka na dada zenu
tutakuwa tayari kwaajili yao.
Wenu mtiifu
Baba
Imma Matukio inaungana moja kwa moja kuomboleza msiba huo na
wawili hao (Idrisa na Wema). Tunatumia fursa hii kuwapa pole wazazi hao waliotegemea
kupata watoto mapacha. Mungu awaweke mahali panapostahili. Tunawaombea subira katika kipindi hiki na kuwataka Watanzania na mashabiki wote wa wool ha kuwa na moyo wa uvumilivu. Mangu awape nguvu na ujasiri katika kipindi hiki
Amina
Amina
No comments:
Post a Comment