Na Mwandishi Wetu, Tanga
WATOTO
wa kiume wenye umri wa miaka sita majina tunalihifadhi amechoma moto
nyumba yao yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 300 kwa kutumia kibiriti
hali iliyosababisha kuteketea yote, baada ya magodoro katika chumba chao
kushika moto ikiwemo vifaa vya magari matairi vilivyokuwemo ndani ya
chumba hicho.
Akizungumza
na Majira mfanyakazi wa ndani Semeni Masele 20 alisema aliona chumba cha watoto
kikiwa kinawaka moto na moshi mkubwa ambapo alilazimika kuwatoa nje akiwemo
Bibi kikingwe mwenye umri wa zaidi ya miaka 100 kisha kuwahifadhi kwa majirani
zao na kulazimika kukimbilia faya kuomba msaada.
Semeni
alisema baada ya kuona hali tete aliwapigia simu Askari wa zimamoto
lakini alipoona namba haipokelewi alilazimika kukondi pikipiki na
kwenda fanya kuomba msaada kwa lengo la kuokoa mali zilizokuwepo ndani.
Tukio hilo
la kusikitisha limetokea juzi majira ya saa 14:30 kijiji cha Mikanjuni
Tarafa ya Ngamiani kati kata ya Mabawa wilayani Tanga ambapo Tanesco na
askari wa kikosi cha zimamoto walifanikiwa kufika katika eneo la tukio na
kuzibiti moto huo usizingile nyumba za majirani ambapo nyumba hiyo
iliteketeza vyumba vinne kati ya vyumba saba.
Uchunguzi wa
awali uliofanywa na Gazeti hili katika eneo la tukio ulibaini kuwa watoto hao
walikuwa wawili ambapo mmoja alikuwa na miaka sita na mwingine saba baada ya
chakula cha mchana waliambiwa na dada yao Semeni walale lakini cha kushangaza
mtoto huyo alikuta box la vibiriti ndani na kuwasha kisha kuchoma box
hilo hali iliyosababisha matairi ya gari yaliyokuwa ndani kuteketea kwa
moto na kusababisha moshi mkubwa.
Kwa upande wake
wakazi wa Mikanjuni walipongeza hatua ya Tanesco kufika kwa wakati kuzima umeme
licha ya kuwa miundombinu ya nyumba ilikwa imekushika moto lakini jitihada
zilionekana ambapokikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuzibiti moto huo mkubwa
ambao ungeweza kuteketeza nyumba za mtaa mzima katika eneo hilo.
“Sisi
wananchi wa mkoa wa Tanga hatutambui namba ya kikosi cha uwokoaji cha zimamoto
pindi majanga yanapotokea hivyo tunaomba kuelimishwa kwa kutangaza namba zao
ili tuweze kunusuru mali wakai wa majanga” walisema baadhi ya wananchi katika
tukio hilo.
Akizungumzia
tukio kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Mihayo Msikhela alisema tukio hilo
limetokea juzi majira ya saa nane mchana baada ya watoto hao kutakiwa kwenda
kulala na dada yao ambaye ni mfanyakazi wa ndani ambapo mtoto wa kiume
alichukuwa kibiriti na kuchoma box kisha moto huo kuteketeza magodoro
ikiwemo viashiria vya vimiminika.
Hata hivyo
kamanda Msikhela aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuweka vitu vya hatari
ndani ya vyumba vya kulala watoto ili kunusuru madhara kama hayo yasitokee.
“Ninawaomba
wananchi wa mkoa wa Tanga kuwa makini wakati wa kuwalea watoto kuondoa thana
ndani ya vyumba vyao vya kulala ili kunusuru madhara pamoja na majanga
yasitokee kutokana watoto ni watu wa kujaribu pindi anapoona kitu anataka
kukitumia bila kuchukuwa tahadhari yeyote.
No comments:
Post a Comment