Tuesday, January 26, 2016

BODABODA AMDANGANYA SHEMEJI YAKE, AMLAWITI

Na Mwandishi Wetu, Tanga

JESHI la polisi mkoani Tanga, linamshikilia mwendesha pikipiki maarufu bodaboda, kwa tuhuma za kumlaghai mke wa kaka yake kwamba anampeleka nyumba ya kulala wageni ili akamfumanie mumewe badala yake akamlawiti baada ya kumlewesha viroba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Tanga, ACP Msikhela Mihayo, alisema tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita majira ya 1:30 usiku huko Donge Jijini Tanga, baada ya bodaboda huyo Aidan Said (26) mkazi wa Mwanzange alimrubuni shemeji yake (jina linahifadhiwa) mkazi wa Msambweni Jijini hapa.

Alisema bodaboda huyo alimweleza shemeji yake huyo kwamba kaka yake ambaye ni mume wa mwanamke huyo,kwamba amekuwa na mazoezi ya kwenda kufanya mapenzi na mwanamke mwingine kwenye nyumba ya kulala wageni iliyopo eneo la mtaa huo wa Donge, hivyo waongozane akamfumanie.

Kamanda Mihayo alisema kwamba baada ya mwanamke huyo kuelezwa hivyo, alikubali kwenda na shemeji yake huyo aliyempandisha kwenye bodaboda hiyo hadi katika nyumba hiyo ya kulala wageni kisha wakaa nje kumsubiri mumewe aje na mwanamke huyo huku wakipata vinywaji.

"Sasa wakiwa pale kwenye nyumba ile ya wageni yule bodaboda alimlaghai shemeji yake kwamba wakati wakimsubiri wanywe pombe hivyo akamnunulia viroba akawa nakunywa, alipolewa alimwingiza kwenye moja ya chumba na kumlaiti," alisema kamanda huyo.

Hata hivyo, ACP Mihayo alisema baada ya tukio hilo polisi walipata taarifa na kisha kumkamata mtuhumiwa ambaye kwa sasa yupo katika kituo cha polisi akihojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani wiki hii kujibu shitaka lake.
Katika matukio mengine watu wawili wamekufa maji katika mtukio tofauti yaliyotokea wilayani Kilindi mkoani Tanga, kufautia kunyesha mvua zilizosababisha madimbwi yaiyoleta maafa ya watu hao kufa.

Kamanda huyo alimtaja Mwajuma Idd mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu wa kijiji cha Kwemigole wilayani Kilindi alipokutwa na wazazi wake amekufa majia kwenye shimo lililojaa maji ambalo lilichimbwa kwa ajili ya matumizi ya choo.

Mtu mwingine Bakari Lugendo (32) kijiji cha Mafisa alikutwa amekufa maji katika shimo lililojaa maji ambalo lilikuwa linatumiwa kufyatulia matofari.


No comments:

Post a Comment