Monday, January 11, 2016

ASKOFU ANGLIKANA ATIMULIWA KWA UFISADI WA MILIONI 521.4

(KUSHOTO) Mchungaji Andrew Kashilimu,ambaye ni Mwenyekiti wa Nyumba ya wahudumua wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) akisoma tamko la Wachungaji hao la kumfzi ya Uaskofu, Askofu Bonifasi Kwangu kwa tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa maadili,katiba ya jimbo na ya kanisa hilo na matumizi mabaya ya madaraka.kulia ni Makamu Askofu, Mchungaji Gerimshom Yoboka. Tamko hilo lilisomwa jana katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicolaus,jijini Mwanza.

Na Daud Magesa, MWANZA

Wachungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN),wamemfukuza kazi Askofu wa kanisa hilo, Askofu Bonifasi Kwangu, wakimtuhumu kwa ufisadi wa zaidi ya sh.521.4,matumizi mabaya ya madaraka,kukiuka kiapo chake, Katiba ya Jimbo na ya DVN.

Wachungaji hao jana walitoa tamko la kumfukuza kazi Askofu Kwangu,wakidai kuwa Kanisa hilo la DVN limekosa imani naye hivyo kuridhia kwa kauli moja kumfukuza askofu huyo.

Mwenyekiti wa Nyumba ya Wahudumu ,Mchungaji Andrew Kashilimu,akisoma tamko la kumfukuza kazi alieleza kuwa, uamuzi huo ulifikiwa baada ya tume iliyoundwa kushughulikia mgogoro wa Anglikana DVN ambayo ilibaini mambo yaliyiofanywa kinyume na askofu huyo.

Mchungaji Kashilimu,katika tamkoa hilo alisema kuwa walikutana Septemba mwaka jana kwenye kikao ambacho kilithibitisha kuwa Askofu Kwangu, hafuati katiba,knuni na taratibu za kanisa la Angalakana Tanzania na amekuwa akiendeleza matabaka miongoni mwa wahudumu na waumini.

Pia, kikao hic ho kilibaini kuwa,alikikuka viapo vyake vya utii,matumizi mabya ya mali na fedha za kanisa,kutoa ajira ndani ya DVN kinyume bila kufuta taratibu za kanisa hilo.

Kutokana na kubaini ukiukwaji huo wa katiba na taratibu za kanisa, kikao hicho cha wachungaji kiliridhia Askofu Kwangu ajiuzulu wadhifa huo kwa maslahi na afya (ustawi) wa kanisa la Mungu,jambo ambalo hakutekeleza.

“Kwa ujumla hali ya huduma ya Mungu ni mbaya ndani ya kanisa la Anglikana-DVN.Mambo haya yamesitirika kwa muda mrefu sasa ni aibu lakini tumelazimika kuyasema.Askofu Bonifasi Kwangu,amekiuka viapo vyake,katiba ya jimbo na katiba ya DVN,matumizi mabaya ya madaraka,mali na fedha za kanisa,ukiukwaji wa maadili na kanuni za kanisa,”alisema Mchungaji Kashilimu kwenye tamkoa hilo.

Ilidaiwa katika tamko hilo kuwa, Askofu Kwangu alihusika katika upotevu wa sh.500 milioni kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya shule ya Kimataifa ya Isamilo inayomilikiwa na kanisa la DVN.Pia,askofu huyo anadaiwa kufungua akaunti binafsi na ya siri katika benki ya Mkombozi Mwanza,ambayo amekuwa akiitumia kwa udanganyifu kujipatia fedha kutoka wahisani mbalimbali kwa jina la Dayosisi.

Aidha, Mchungaji Kashilimu aliendelea kusema katika tamko hilo kuwa, Askofu Kwangu alichukua USD 3000 sawa na fedha za Kitanzania sh.6,000,000 kutoka kwa Mhasibu wa shule ya Isamilo kwa ahadi ya kuzirejesha.

Ilielezwa katika tamko hilo kuwa,Mhasibu huyo alipomdai ili arejeshe fedha hizo, alimfukuza kazi fedha na hakuweza kuzirejesha hadi sasa,lakini pia alishindwa kuwasilisha fedha za zilizochangwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Kuu za ada ya Jimbo.

Anadaiwa kujipatia sh. 15,364,560 kutoka kwa mhasibu wa Dayosisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano (2008-2012) na kushindwa kuzirejesha hadi sasa,ambapo anatuhumiwa kuajiri Mhasibu wa shule ya Isamilo asiye na sifa, kinyume cha taratibu (DC),akilenga kuficha uovu katika eneo la fedha.

Mchungaji Kashilimu aliendekea kueleza kuwa, askofu huyo aliajiri watumishi wa shule ya Isamilo na ofisi za Dayosisi bila kufuata taratibu, kinyume na taratibu za utumishi wa ajira za DVN na kubadili matumizi ya shule ya Bibilia Nyakato-Mwanza kuwa sekondari isiyo na tija kwa kanisa la Mungu.

Anadaiwa kusababishia Dayosisi idaiwe nazaidi ya sh.60 milioni na watumishi waliofukuzwa kazi kinyemela au waliosimamishwa kazi,lakini pia ameuza gari la Dayosisi lililochangiwa na waumini wa kanisa hilo na fedha hizo hazijulikani zilipo.

Tuhuma zingine zinazomkabili askofu huyo ni kukosekana na kwa taarifa ya mapato na matumizi katika kipindi chote cha miaka 8 alichohudumu akiwa kiongozi na Askofu wa Kanisa hilo na anakuwa wa pili kufukuzwa Uaskofu wa Kanisa hilo la DVN,akitanguliwa na Askofu John Changae aliyefukuzwa Machi 2007 .

Juhudi za gazeti hili kumpata Askofu Kwangu kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata kauli yake kuhusu madai hayo, ziligonga mwamba baada ya simu yake kutokuwa hewani.Lakini habari ambazo gazeti hili imezipata punde zinaeleza kuwa, yuko safarini nchini Marekani, kwa shughuli zake binafsi.


No comments:

Post a Comment