Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu, kutoka kushoto Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Makamba, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Msaidizi wa Balozi, Ubalozi wa UFINI ambao ni wafadhili wa mama misitu, Simo-Pekka Parviainen na Ofisa Mradi Ubalozi wa Finland, William Nambiza.
SOMA ZAIDI. . .
Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa chokozi katika uzinduzi wa mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini uliofanyika Hoteli ya New Africa Dar es Salaam leo.
Maofisa mbalimbali waliopo kwenye mradi huo wa Mama Misitu wakiwa katika uzinduzi huo
Mshauri wa Ufundi Weizara ya Maliasili na Utalii, Thomas Sellaine (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Hapa Wanahabari mbalimbali wakifuatilia kwenye uzinduzi huo.
MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia
televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua
mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa
endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.
Vipindi hivyo mfululizo vimetengenezwa katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro ikiwa ni
sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu
Tanzania (MJUMITA), Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG),
Shirika la Kuendeleza Teknolojia za Asili (TATEDO) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuleta mabadiliko na kurasimisha sekta ya mkaa iweze kutoa ajira endelevu na kipato kwa jamii za
vijijini na mijini.
Inakadiriwa kuwa mkaana biashara za kuni huzalisha takriban (dola bilioni 1) za mapato kwa zaidi ya wazalishaji,wasafirishaji na wafanyabiashara laki tatu (300,000) katika mwaka 2012.
Mahitaji ya mkaa nchini Tanzania yameongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa.
Mkaa endelevu ni mkaaunaozalishwa kwa njia endelevu kutoka katika Misitu ya Hifadhi ya Jamii bila
kuchangia ukataji miti na uharibifu wa mazingira. Hata hivyo, uzalishaji wa aina hii ya mkaa bado haujajulikana. Kampeni hii mpya ina lengo la kuleta mabadiliko kupitia ubunifu wa vipindi mfululizo vya runinga ambavyo vimezinduliwa leo.
Nishati zitokanazo na tongamotaka (biomas) ni nishati muhimusana nchini Tanzania itakayoendelea kutumika angalau zaidi ya miaka 20 ijayo.
Kwa sasa, mkaa mwingi huzalishwa kinyume na utaratibu kutoka katika misitu ya
hifadhi na misitu ya vijiji isiyo na mipango ya matumizi endelevu. Kutokana na
usimamizi hafifu wa uzalishaji wa mkaa, imesababisha ukataji miti na uharibifu
wa misitu kuongezeka nchini Tanzania.
Kampeni ya Mama Misitu na washirika wake (TFCG na MJUMITA)
inalenga kuleta mabadiliko katika sekta ya mkaa kutoka tatizo kuwa fursa kubwa
muhimu. Hivyo, vipindi vya runinga vya Mama Misitu pamoja na jumbe muhimu za
mawasiliano zitasambazwa nchini Tanzania ili kuibua mjadala wa pamoja juu ya
kuboresha utawala bora wa rasilimali misitu na kuleta faida kwa watanzania.
Mama Misitu ni kampeni ya mawasiliano yenye lengo la kuboresha utawala bora wa misitu ya Tanzania na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu ili watu wa Tanzania wanufaike zaidi na rasilimali misitu zao.
No comments:
Post a Comment