Thursday, September 03, 2015

AKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUDUMU YA AU, ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Wanawake na Watoto Zanzibar, Zainab Omar, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha, kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu, ulioanza jana Novemba 4, katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.

SOMA ZAIDI...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mkuu wa Mkoa Arusha, Mulongo Magesa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Balozi Liberata Mulamula, wakati akiingia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC Mkoani Arusha kufungua mkutano wa wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu. Mkutano huo umefunguliwa jana Novemba 4.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa AICC, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo eliofunguliwa Nov 4, jijini Arusha.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa AICC, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo eliofunguliwa Nov 4, jijini Arusha. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Wizara za Maendeleo ya Wanawake na Watoto, wa Nchi za Maziwa makuu , uliofunguliwa jana Nov 4, katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.


Picha na Muhidin Sufiani-OMR


No comments:

Post a Comment