Wednesday, June 18, 2014

TATHMINI YA KOMBE LA DUNIA: TIMU ZOTE 32 ZIMESHACHEZA MECHI, NINI KINAFUATA?

Timu zote 32 za nchi mbalimbali duniani zilizoko nchini Brazil kushiriki kinyang'anyiro cha finali za kombe la dunia, ili kumtafuta bingwa wa dunia mwaka 2014 katika mchezo wa soka, zimeshacheza mechi zake za kwanza.

Inafurahisha kuona jumla ya magoli 49 yameshafungwa ikiwa ni wastani wa magoli 3 kila mechi. Sasa ni nini kinafuata? Tuangalie mechi zijazo. Kinyume na mategemeo ya wengi timu ambazo zilitegemewa kufanya(Spain, Portugal, ) maajabu ndio zimebwagwa na nyingine kuishia kusuasua (Brazil, Nigeria, Cameron).
Nchi za Afrika ziko katika wakati mgumu zaidi kutokana na matokeo mabovu mpaka kufikia sasa. Jumla ya timu 5 kutoka barani Afrika zimeingia katika kinyang'anyiro hicho cha kombe la dunia Brazil 2014, timu hizo zikiwa ni Cameroon, Ivory Cost, Nigeria, Ghana na Algeria. huku timu moja tu ndio mpaka sasa ndio iliyoshinda ambayo ni Ivory Cost ilipoichapa Japan 2 - 1.



No comments:

Post a Comment