Shirika la habari la nchini Marekani, Fox News kupitia televisheni, limeitaja Tanzania kuwa moja ya nchi zenye mvuto wa kuvutia zaidi na kwamba ni ya kutembelea. Pamoja na Brazil, Australia, Marekani na China, Tanzania ilishika nafasi ya nne ulimwenguni.
Fox News ilitoa sababu :” Tanzania ina hifadhi ya mbuga
nyingi ambazo ni ukumbwa kuliko jimbo la Texas, ikiwa ni pamoja na mbuga ya
Serengeti yenye ukubwa maili za ujazo 6,000 zenye mchanganyiko wa wanyama kama
nyumbu, swala, pundamilia pamoja na wanyama wakali. Tukio la kuhama wanyama
linatokea kila mwaka ni tukio kubwa zaidi lilibaki duniani linalohusisha
uhamaji wa wanyama duniani.
Tanzania pia ina mlima mrefu kuliko yote Afrika, mlima
Kilimanjaro, ambao una misitu minene katika miteremko yake ambayo ni hifadhi
kubwa ya viumbe vilivyoko hatarini kutoweka.”
Ukiacha safari za utalii na kupanda mlima Kilimanjaro,
tunakuhakikishia kuwa ina mambo mengine mengi tu. Utajiri wa tamaduni
mbalimbali pamoja na kisiwa kizuri katika bahari ya Hindi ni sababu nyingine
itakayo kufanya utembelee Tanzania haraka uwezavyo.
No comments:
Post a Comment