BREAKING NEWS:BARABARA YA MOROGORO KUTOKEA SHEKILANGO YAFUNGWA
Kipande cha Barabara ya Morogoro kufungwa kuanzia leo tarehe 10/06/20124. Katika tangazo lilitolewa katika vyombo vya habari, kipande hicho kitafungwa ili kukamilisha ujenzi wa mabasi yaendayo haraka.
Kipande kinachotegemewa kufungwa ni kile cha kuanzia makutano ya Sam Nujoma hadi Shekilango. Kufuatia tukio hilo, watumiaji wa barabara hiyo wameshauriwa kutumia njia mbadala kama inavyooneshwa katika ramani ya tangazo hilo.
Kama inavyoonesha ramani hiyo, watumiaji wa barabara watakunja kuingia kushoto kama unatokea Kimara na kisha utafuata maelekezo na kisha kutokea barabara ya Shekilango kuelekea Manzese.
Strabag na wadau wengine wa barabara wameomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
No comments:
Post a Comment