Huku wakikiri shambulizi hilo wametoa onyo kwa watalii kukoma kuja Kenya. Taarifa ya kundi hilo ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Kenya kwa kufanya msako dhidi ya waisilamu kwa njia ya kuwafunga kiholela na kuwaua wahubiri wa kiisilamu.
Baadhi ya walioshuhudia mashambulizi hayo wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
No comments:
Post a Comment