Katibu wa Azam Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’
aliongea na mwandishi wetu leo na kusema kwamba wamefuata taratibu zote kabla
ya kumsainisha
mchezaji huyo, na kufanikiwa kumalizana na klabu yake, AS
Cannes ya Ufaransa.
“Kama inavyofahamika, mchezaji huyu alihamishwa kutoka Simba
kwenda AS Cannes mwaka jana, kwa hivyo nasi tumemsajili kutoka timu hiyo,
lakini asilimia fulani ya fedha, ambazo tutawalipa Simba,”amesema Nassor.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba Zacharia Hans Poppe amesema; “Hatuna tatizo na Kapombe, awaambie
Azam walete asilimia 40 yetu
katika fedha walizotoa kumnunua huko Cannes, na sisi
tutanunua wachezaji wengine wazuri tu hata wawili kwa hiyo fedha,”.
Tayari Kapombe alikuwa amekwishajiunga na Azam tangu Machi
mwaka huu baada ya kugoma kurejea Ufaransa tangu Novemba mwaka jana aliporejea
kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.
Kapombe aliyezaliwa Januari 28, mwaka 1992 aliibukia katika
timu ya vijana ya Polisi Morogoro kabla ya kusajiliwa na Simba mwaka 2011,
ambako alicheza hadi Agosti mwaka jana alipojiunga na Cannes.
Simba SC ilimtoa mchezaji huyo bure AS Cannes kwa
makubaliano akiuzwa klabu nyingine, itapata mgawo mzuri. Hata hivyo, baada ya
kugoma kuendelea kuchezea klabu hiyo ya Daraja la Nne, Simba SC ilitakiwa
kulipa Euro 33, 000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake
huyo.
Kapombe anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na mabingwa hao
wapya wa Ligi Kuu, baada ya beki Abdallah Kheri kutoka Zimamoto ya Zanzibar
kiungo Frank Domayo na washambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu kutoka Yanga na
Ismaila Diarra kutoka Mali.
No comments:
Post a Comment