Saturday, April 26, 2014

POLISI: MWANAMKE AUZA DAWA ZA KULEVYA AKIWA ICU

Polisi wanasema, mwanamke mmoja amefanikiwa kuuza dawa za kulevya na kujipatia maelfu ya dola za Kimarekani akiwa hospitali katika chumba cha wagonjwa mahututi. Mwanamke huyo ambaye ni raia wa Marekani na mkazi wa Pennsylvania, bado yuko hospitali wageni wake wakiwa wamezuiwa kumuona.

Mwanamke huyo ameshtakiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya na kudaiwa kuuza dawa aina ya heroine huku akiwa hoi kitandani katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), polisi wamesema.

Lori Sullenberger, 38 mkazi wa Youngwood, Pa. alianza kupata wageni waajabu waliokuja kumtembelea hospitali katika chumba chake katika hospitali ya Excela Westmoreland, alieleza msemaji wa hospitali.
Kwa mujibu wa ripoti ya Action News 4, kutokana na wageni hao Polisi walianza kufanya uchunguzi, wapelelezi walinunua mifuko 30 ya dawa aina ya heroin yenye thamani ya dola 3,800(sawa na shilingi za Tanzania 6,228,200) huku wakikamata $1,420(sawa na shilingi za Tanzania 2,327,382) fedha taslim kutoka katika chumba hicho.
Sullenberger alikuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa usiohusiana na matumizi ya dawa za kulevya, kwa mujibu wa polisi. Polisi wanasema mwanamke huyo alikuwa na simu kadhaa katika chumba chake ambazo ziliita kila wakati, na wageni wake wengi hawakujua jina lake la mwisho.
“kwakweli hili ni rukio la kipekee kuwahi kutokea, kuuza dawa za kulevya kutokea ICU, sehemu ambayo watu wanajaribu kuokoa maisha” polisi mmoja alieleza.
Sullenberger bado yuko hospitali mpaka jumanne wiki hii, wakati polisi wakishughulikia taratibu za kumkamata yeye pamoja na mpenzi wake na mtu mwingine wa tatu ambao wanadaiwa kununua au kukutwa na dawa hizo.


No comments:

Post a Comment