Monday, April 14, 2014

BUNGE MAALUMU KUCHANGIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO ZAIDI YA SH.180 MILIONI

Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma limeridhia kuchangia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali zinazoendelea.

Hoja hiyo ilitolewa na Mbunge na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Kazi Maalumu, baada ya kutoa taarifa ya ajali iliyotokea ambayo jana, iliyomhusisha Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Afande wa Kikosi Maalum, Suleiman Kova, Mkuu wa Mkoa wa DSM, Said Meck Sadik.

Mh. Mwandosya alishauri Bunge hilo maalum lichangie kwa kutoa posho zao za siku moja ambazo zitafikia shilingi za kitanzania zisizopungua milioni 180.

Pamoja na kukubaliwa kwa wabunge wengi wa bunge hilo, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samwel Sitta alipokea hoja hiyo na kuahidi kuiwakilisha kwa wahusika ifanyiwe kazi kwaajili ya utekelezaji

TOA MAONI YAKO CHINI HAPO TAFADHALI


No comments:

Post a Comment