Monday, April 14, 2014

ATHARI ZA KUTISHA ZA MVUA BARABARA YA KILWA ENEO LA KONGOWE

Wakazi wa eneo la Kongowe wakiangalia sehemu ya madhara yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea nchini na hivi ndivyo daraja lilivyokatika na kusababisha msongamano na kushindwa kupitika katika barabara ya Kongowe, Wilaya ya Temeke

JUU: Hapa ni eneo lililokuwa linatumika kuhifadhi mabomba ya kusafirisha gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam, hayo ni baadhi ya malory yaliyokuwa yanasafirisha mabomba hayo,
CHINI: Ni geti la kuingilia katika eneo hilo pamoja na ofisi ndogo nyuma ya geti hilo kama eneo hilo linavyoonekana baada ya mvua kubwa kunyesha



 Mtu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja bila kujali usalama wake, akijaribu kuogelea ili kwend kuokoa tanki la maji (SIMTANK) lililozolewa na maji, hata hivyo mtu huyo hakufanikiwa kwani maji yalikuwa na kasi kubwa (Picha ndogo) akijitahidi kupambana na maji
Wapita njia wakishangaa daladala lililoamua kutanua ili kukwepa foleni likiwa limekwama katika barabara ya Kilwa eneo la Kongowe.



No comments:

Post a Comment