Thursday, March 13, 2014

YANGA YANGURUMA, YAMJIA JUU MEYA WA ILALA, YAMPA SIKU 5 TU

Uongozi wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, umetoa siku tano kwa Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa kuwapatia kibali cha kutengeneza uwanja wa Jangwani(PICHANI KUSHOTO).

Akizungumza na waandishi Katibu wa Baraza la Wazee, Mzee Akilimali alisema kuwa wanashangaa kwanini kamati ya madiwani inawawekea kauzibe katika suala hilo.

Alisema klabu ya Yanga iliomba kibali tangu mwezi wa sita mwaka jana hadi leo hawajapata na kwamba ni jambo la kushangaza sana. 

SOMA ZAIDI . . .

"Sisi kama wana Yanga tunatoa tamko kwa serikali iwe imetoa kibali kabla siku 5 hazijaisha lasivyo tutafanya maandamano mji mzima hapa Dar es Salaam."

Akilimali alisema maandamano hayo yataelekea moja kwa moja kwa Mkuu wa Mkoa ama Rais wa nchi. Uwanja wa Jangwani kama unavyoonekana pichani, ni uwanja ambao hauna kiwango na haufai kufanyia mazoezi, haswa kwa timu yenye hadhi kubwa kama Yanga. 


No comments:

Post a Comment