Wednesday, March 26, 2014

YANGA 5 PRISON 0,MPIRA UMEKWISHA, YANGA INAENDELEA KUSHIKA NAFASI YA 2

Katika mechi ya kukamilisha mzunguko wa ligi kuu ya Tanzania bara maaru kama Vodacom Premium League, leo wazee wa Jangwani Yanga wameshuka dimbani kukipiga na walinzi wa magereza wa jiji la Mbeya, Tanzania Prisons.

Mechi hiyo inayoendelea katika Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam, kipindi cha kwanza dakika ya 20 Yanga imepata bao kupitia mchezaji wao Emmanuel Okwi ambaye alipat mpira wa faulo na kuachia shuti kali na moja kwa moja kutinga wavuni.


Dakika ya 34 Prison walipata penati penati ambayo ilipigwa na mchezaji wake Lugano Mwangama na kukosa. Penati hiyo ilitokana na Oscar Joshua kumsukuma mchezaji Frank katika eneo la hatari.
Wakati mpira huo unaendelea dakika ya 37 Yanga walipata bao la pili lililofungwa na Mrisho Ngasa baada ya kupokea pasi ya maana kutoka kwa Hussen Javu.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika Yanga inaongoza kwa magoli 2 huku Prisons ya Mbeya ikiwa haijapata kitu, katika dakika 20 za mwisho Yanga walifanya mashambulizi makali katika lango la Prisons lakini ikapoteza magoli mengi.
Katika kipindi cha pili Yanga yapata bao la tatu kupitia mshambuliaji wake Hamisi Kiiza katika dakika ya 67. Hamisi Kiiza ameingia katika kipindi cha pili akichukua nafasi ya mchezaji Emmanuel Okwi ambapo alipokea pasi nzuri kutoka kwa Simon Msuva.

Katika daika 76 Yanga ilipata penati kutokana na mchezaji wa Prison kumchezea madhambi Hussen Javu katika eneo la hatari na kusababisha penati iliyozaa goli lililofungwa na Nadir Haroub Canavaro na kusababisha Yanga kupata bao la nne.

wakati mpira unaendelea katika dakika ya 88 Yanga wanajipatia bao la 5, goli safi lililofungwa na Hamisi Kiiza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Hussen Javu. Yanga 5 Prison 0

Mpira umekwisha na matokeo ni Yanga 5 Prison 0, na kwa matokeo hayo, Yanga itaendelea kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara huku wakiwa na jumla ya point 46 nyuma ya Azam ambao kwa ushindi wake wa goli 2 - 0 dhidi ya Mgambo JKT, wanashikilia nafasi ya kwanza kileleni

No comments:

Post a Comment