Monday, March 17, 2014

NDAUKA AJIPA UBAROZI WA USAFI, ASHIRIKIANA NA WASANII KUSAFISHA JIJI



Msanii wa filamu nchini Rose Ndauka akifanya usafi mtaa wa Rumumba eneo la Mnazimmoja huku akishirikiana na baadhi ya wasanii wenzake, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kufanya usafi.

Rose ameamua kujitolea kwa jamii kwa ajili ya kufanya usafi ili jamii itambue kuwa kufanya usafi ni jukumu la kila mmoja na siyo kusubili halmashauri au serikali, ambapo zoezi hilo ni endelevu na atalifanya nchi nzima.

Mbali na kuhamasisha usafi pia msanii huyo alizindua jiko la kuchoma taka.

Msanii wa filamu Rose Ndauka (wa tatu kulia) akiwa ameambatana na baadhi ya wanafunzi na wasanii wenzake pamoja na Meya wa Ilala Jerry Slaa (wa tatu kushoto)




No comments:

Post a Comment