Tuesday, March 18, 2014

MSANII MAARUFU WA DANCEHALL, VYBZ KARTEL AUA NA KUKATAKATA MWILI

Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dancehall reggae, Vybz Kartel na wenzie watatu wamekutwa na hatia kwa kosa la mauaji alhamisi 13/03/2014 katika kesi ya mauaji iliyokuwa ikiendeshwa chini ya ulinzi mkali katika mahakama kuu ya jijini Kingston, nchini Jamaika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, polisi wa jiji la Kingston wakiwa wamejihami kwa kuvaa mavazi maalumu pamoja na vizuizi mitaani tayari kwa lolote, jopo la wajumbe 10 kati ya 11wa baraza la wazee la mahakama, kwa pamoja waliwatia hatiani Vybz Kartel na wenzie watatu katika shitaka la mauaji ya Clive ‘Lizard’ Williams.

Mmoja kati ya walioshtakiwa aliachiwa huru baada ya kuonekana hakuwa na kosa lolote linalo husiana na mauaji hayo.

Katika hali ya kushangaza, mmoja kati ya wajumbe wa baraza la mahakama alikamatwa siku ya alhamisi jioni kwa kosa la kutaka kuhonga baraza hilo ili kushawishi baraza kumuachia huru Kartel.

SOMA ZAIDI . . .

Mwendesha mashtaka alieleza katika kesi hiyo kuwa Williams alipigwa mpaka kufa nyumbani kwa Kartel mwezi Agosti 2011 baada ya kuhojiwa kuhusiana na bunduki mbili zilizopotea.

Imeelezwa kuwa mwili wake haukuwahi kupatikana. Polisi walitoa ushahidi wa ujumbe wa simu kutoka katika simu ya Kartel ukieleza kuwa Williams alikatwakatwa vizuri kiasi kwamba mwili wake hautoweza kupatikana.

Siku moja kabla kesi hiyo kuanza kusikilizwa, polisi waliweka ulinzi mkali na kufunga mitaa yote inayozunguka Mahakama hiyo ilikuondoa usumbufu wowote utakaoletwa na mashabiki wa msanii huyo.

Pamoja na udhibiti huo, muda mchache kabla ya kesi hiyo kuanza kutolewa maamuzi, kiasi cha watu 200 walivunja uzio na kupenya huku wakipiga kelele “free Kartel!” wakimaanisaha Kartel aachiwe huru.
Mwanasheria aliyekuwa anawatetea washtakiwa, Tom Tavares-Finson aliliambia baraza la wazee wa mahakama kwamba mashtaka dhidi ya Kartel sio ya kweli na hayastahili kwa kuzingatia ushahidi ulioelezwa pamoja na diski yenye ushahidi uliohifadhiwa kupotea. Baada ya uamuzi huo, mwanasheria alipanga kukata rufaa.

Mwaka jana, kesi nyingine ya mauaji dhidi ya Kartel na wenzie wawili, ilitupiliwa mbali baada ya ushahidi kudhibitisha kuhusika kwa watatu hao katika mauaji ya mfanyabiashara Barrington “Bossy” Burton mwaka 2011 kukosekana.

Kartel ambaye jina lake halisi ni Adidja Palmer, amekuwa jela kwa takribani miaka 3, lakini miziki yake imekuwa ikichezwa kwa kiasi kikubwa na vijana wengi nchini Jamaika na haswa wale wanaoishi katika maeneo ya hali ya chini wanaomuona Vybz Kartel kuwa ni shujaa.


No comments:

Post a Comment