Wednesday, March 26, 2014

MAKUBWA: HOTELI INAKUWEZESHA KULA CHAKULA NA WAFU (SOMA NGALIA PICHA)




Mgahawa mmoja nchini India unakuwezesha kula chakula na wafu…najua unashangaa, ndio wafu…watu waliokufa. Hoteli hiyo imejengwa makaburini na kuzunguka makaburi ya zamani, hivyo makaburi yako ndani kama unavyoona pichani.

Mmiliki wa hoteli hiyo iliyoko Ahmedabad, kule wanakotoka Wahindi wanaoongea kiGujrati, nchini India, anasema biashara ya makaburini inalipa sana.

Krishan Kutti aliamua kujenga na kuyaacha makaburi hayo na kuyatunza badala ya kubomoa ili ajenge hoteli yake. Lakini ukiacha ujenzi wenye mvuto ndani ya hoteli hiyo, hoteli hiyo imekuwa maarufu sana kwa watu kujirusha.

Yeye anasema makaburi hayo yamekuwa kivutio kikubwa na yanaleta bahati nzuri. Biashara yetu imeendelea kufanikiwa sababu ya makaburi hayo. Yanawapa watu mvuto tofauti. Tumeyaacha kama yalivyo, wateja wetu wala hawana shida.


SOMA ZAIDI . . .

Lakini Kutti hajui hayo makaburi ya nani, yani kina nani wamezikwa humo. Wakazi wanaozunguka eneo hilo wanadai kuwa ni ya wafuasi waliozikwa karne ya 16 wa mtume Sufi ambaye naye mabaki yake yamehifadhiwa karibu na eneo hilo.

Zaidi ya dazeni moja ya makaburi yamo ndani ya hoteli hiyo na kila moja limezungushiwa grili za chuma ili kuyalinda. Kila asubuhi mapazia yanapofunguliwa, wafanyakazi wa hoteli hufuta vumbi katika kila kaburi na kisha kuyapamba kwa kutumia maua ya asili.

“Tunaanza siku kwa kutoa heshma kwenye makaburi hayo, kisha tunayafuta vizuri alafu tunayafunika na kitambaa alafu tunaweka maua mazuri, ni muhimu sana kuheshimu wafu” alisema Kutti.

"Wateja kwa upande mwingi hawajali uwepo wa wafu katika hoteli yetu, wanakuja kunywa chai na mikate bila wasiwasi wowote" alimaliza Kutti.





No comments:

Post a Comment