Katika taarifa iliyotufikia muda si mrefu, imeeleza kuwa
kampuni mbili kubwa kuliko zote nchini Marekani za kutengeneza bia zimejitoa
katika udhamini wa matembezi ya hiari ya siku ya Mtakatifu Patrick (St.
Patrick's Day) kwa sababu wasenge na mashoga hawatoruhusiwa kujitambulisha
katika matembezi hayo.
Katika taarifa iliyotolewa muda si mrefu na shirika la
habari la CNNMoney(CNN) lililoko New York, imedai kuwa Sam Adams, ambaye
ndio mmiliki wa kampuni ya kutengeneza bia ya Boston Beer Co. imebadili mawazo
na kwamba haitafadhili matembezi hayo yanayotarajiwa kufanyika kesho jumapili.
SOMA ZAIDI . . .
SOMA ZAIDI . . .
Nalo shirika linalozalisha bia ya Heineken, ambayo
pia ni maarufu nchini Tanzania na hupendwa na watu wengi ilijitoa katika
kufadhili wa matembezi ya hisani ya Ney York City toka jumatatu.
“tunaamini katika usawa kwa kila mmoja” alisema msemaji wa
Heineken tawi la Marekani.
Sam Adams inadaiwa kujaribu kuwabembeleza waandaaji wa
matembezi ya Boston kubadilisha sharia zao na kuwaruhusu kundi la LGBT (wasagaji, mashoga, mabasha na waliobadili jinsia)
kushiriki matembezi hayo.
“tulitegemea kufikia makubaliano kuruhusu kila mtu kushiriki
bila kujali hali yake kushiriki katika matembezi hayo” kampuni hiyo ilieleza
katika taarifa yake, “lakini kutokana na hali ya makubaliano ilivyo sasa, hilo
halitowezekana”
nao waandaaji wa matembezi hayo, The South Boston Allied War
Veterans Council, walisema katika taarifa yao iliyoko kwenye tovuti yao kuwa
haizuii LGBT(Lesbians, Gay Bisexual na Transsexual) kushiriki katika matembezi hayo, bali
hawaruhusiwi kuonesha au kutangaza na kubeba mabango yanayowatambulisha.
Ilieleza kuwa mashoga na wasagaji wakongwe waliotaka
kushiriki maandamano kama sehemu ya kundi la wakongwe wa LGBT bado wanaweza kushiriki kwa masharti kwamba
hawatatambulika kuwa ni mashoga na kuvaa tisheti na alama zinazoonesha hivyo.
“tunawakaribisha wote kuja kusherehekea tukio hili la
kihistoria, lakini ni lazma tuendelee kushinikiza sharia kwa ajili ya usalama
wa kadamnasi” walisema waandaaji.
Hata Meya wa jiji anadukuduku, Meya wa jiji la New York Bill
de Blasio amegomea matembezi hayo, wakati Meya wa jiji la Boston Martin Walsh
ameripotiwa akijaribu kubembeleza waandaaji kubadilisha sharia kabla hajafanya
maamuzi.
No comments:
Post a Comment