Monday, February 03, 2014

WAFANYAKAZI WA CCBRT WAFUNGUA KESI


WAFANYAKAZI 430 wa vitengo mbalimbali wa Hospitali ya CCBRT wamefungua kesi ya madai namba 843/13 dhidi ya uongozi wa hospitali hiyo Mahakama Kuu Kitengo cha kazi wakiiomba mahakama iwaeleze mishahara wanayolipwa na serikali ni halali au si halali.

Akizungumza nje ya mahakama, mmoja wa wafanyakazi na Katibu wa waliofungua kesi, Achile Lugala, alisema kuwa Novemba, mwaka 2007 hospitali hiyo ilipewa hadhi ya juu na kuwa 'Super Specialist Hospital -Eastern Zone ambapo mishahara ya wafanyakazi ilipanda na ilikuwa inatolewa na serikali.

Alisema kuwa toka mwaka huo hadi sasa wafanyakazi hao wameendelea kupewa kiwango cha zamani cha mishahara  na hospitali hiyo wakati wanatakiwa kupewa kiwango kilichopandishwa na kinacholipwa na serikali.

Alisema kuwa kabla ya kufikia hatua ya kwenda mahakamani walifanya vikao mara mbili na uongozi wa hospitali hiyo pamoja na Mwenyekiti wa Bodi lakini hawakufikia muafaka.



"Wafanyakazi 47 tumefungua kesi ambapo tunawawakilisha wafanyakazi 430, tumeamua kufungua kesi dhidi ya uongozi wa CCBRT, tunakata mahakama itusaidie kujua hiyo mishahara tunayolipwa na serikali ni halili au si halali," alisema.

Achali, alisema kuwa mishahara imetofautiana kwa kila mfayakazi wapo wanaopokea sh.1,000,000 na wapo wanaolipwa hadi sh. milioni 3,000,000 kwa mwezi," alisema.

Aliongeza kuwa wanapewa fomu za mishahara na serikali zinazoonyesha viwango vya mishahara

lakini uongozi wa hospitali umekuwa haufuati utaratibu wa fomu hizo hivyo wanapinjwa mishahara yao.

Kesi hiyo namba 843/13  ipo chini ya Jaji Msuri hata hivyo imeahirishwa hadi Februari 27, mwaka huu ambapo CCBRT kupitia wakili wake kampuni ya Imma imeomba kwenda kuongea na mteja wao kwa ajili ya vielelezo  na kwa upande wa  wafanyakazi hao wanawakilishwa na Kampuni ya Uwakili ya MNL.




No comments:

Post a Comment