Monday, February 03, 2014

UPINZANI WASUSIA UCHAGUZI, HATA HIVYO UCHAGUZI ULIENDELEA


Uchaguzi huo ulifanyika licha ya kususiwa na chama kikuu cha upinzani nchini Thailand.

Asili mia kumi ya vituo vya kupigia kura vilifungwa kutokana na shinikizo la waandamanaji wanaopinga utawawala wa waziri mkuu Yingluck Shinawatra.Kiongozi wa waandamanaji Suthep Thaugsuban ameitisha maandamano zaidi kukaidi utawala wa Shinawatra.

Zaidi ya wapiga kura milioni sita wengi katika maeneo ya mji mkuu Bangkok na kusini mwa taifa hilo, hawakushiriki zoezi hilo kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini.

Licha ya hayo Waziri Shinawatra alionekana kufurahia ufanisi wa zoezi zima la uchaguzi.


Yingluck alisema, ''Ni vyema kufahamu kuwa Thailand inaongozwa kwa misingi ya Demokrasia . Kura hizi ni njia mwafaka ya kusuluhisha migogoro yetu".

Kingozi wa upinzani, Suthep Thaugsuban, aliwaambia wafuasi wake kuwa chama kinachotawala cha Puea Thai party hakitashinda idadi ya chini ya viti vya uwakilishi bungeni vitakayokiwezesha chama hicho kufungua bunge lijalo.

Suthep Thaugsuban alisema, "Wanaendelea kuishinikiza tume ya uchaguzi kuendelea mbele na uchaguzi huu haswa katika maneo yanayokumbwa na msukosuko. Sijui itawachukua muda gani kukamilisha zoezi hili lakini nina hakika kuwa hawatopata viti 475 vya uwakilishi vinavyohitajika kufungua vikao vya bunge".

Uchaguzi huu unafanyika licha ya upinzani nchini humo kufanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa Bangok, mbali na kukaidi amri ya polisi kuanzia mwezi Novemba, wakipinga hatua ya waziri mkuu Shinawatra kutaka kufanya maadiliko ya katiba.

Mabadiliko hayo yangemruhusu kakake, Thaksin, aliyekuwa waziri wakati mmoja kurejea nchini humo.

Thaksin yuko uhamishoni tangu mwaka 2008 alipotoroka kuepuka kufikishwa mahakamani kwa kesi ya ubadhirifu wa mali ya umma. (BBC)

No comments:

Post a Comment